Mimi nashangazwa na Mapindizi haya ya Watanganyika akina Warioba kuto kuheshimu haki na maoni ya Wananchi wa Zanzibar kwa kushurudisha mamudhi yao na kupinga mamuzi ya Wananchi wa Zanzibar walio wengi.
ikiwa Warioba (Kikwete) alikua na Lengo la kunusuru Muungano au ccm basi ilikua aheshimu 60% za Wananchi wa Zanzibar, sio kufanya upendeleo wa 61% ya watanganyika kuwapa Tanganyika huku kuwanyima 60% Mkataba.
Alicho fanya warioba nikuheshimu mamuzi ya upande moja na kutuletea mgogoro mpya hili ni kosa jengine lakutumia Mabavu ya uongozi.
Walichotaka Wazanzibar sio kuibuliwa Tanganyika, nikujadiliwa Muungano wenyewe kwa watu wa Pande zote mbili za Muungano kuwa wanautaka au vipi? Wananchi Wa Zanzibar walipiga kelele sana kusema kama munataka kuandika katiba mpya kwanza tujadili Muungano wenyewe ulozaa katiba sio kujadili katiba halafu Muungano huu ni mgongano mpya na Wananchi wa Zanzibar tunaapa hatutokubali.
Huu uliotumika ni upendeleo wa upande moja kuwapa na mwengine kunyimwa,Wazanzibar hawakuitaka Tanganyika ,Tanganyika ni yenu sie tuna yetu.
Sisi Kujadiliwa kwanza Muungano mukakataa na badae wananchi walio wengi walitaka Muungano wa Mkataba vile vile mumepinga maoni yao lakini ya Watanganyika kutaka Tanganyika ibuliwe Mumekubali Warioba.
Hili ni kosa jengine lakulazimishana na si hivyo tu, mumezidi kuibinya Zanzibar ili itii amri tena kwa kupoteza mamlaka yake kinguvu, katu hili hatutoliruhusu kutokea wakati wa kuburuzana umepitwa.
Tanganyika wao watakua na serikali 2 sasa, maana hii ya muungano headqurters zote zipo kwao, na hii mpya ndo yale yale.
Wazanzibari wanaona maslahi yao katika muungano hayaZingatiwi; Mambo ya Muungano yanasaidia BARA peke yake na ndivyo itakavyo kuwa katika Draft ya Warioba.
Kiukweli mataifa ya nje yanaiangalia Tanzania kama Tanganyika iliyo badilika jina tu, maana mamlaka makubwa yote ya nchi mbili hizi yani Tanganyika na Zanzibar yamo kwenye Muungano na sio nchi mbili hizi.
Sasa Draft ya Warioba hapa nikujua kuwa Serekali ya Sherekisho(Muungano) haitakua na mtazamo wa ki shirikicho itakua ni ya wingi wa Watanganyika kutumia Turufu ya wingi wao tena ya Muungano kwa kujimarisha.
Hakuna shaka tumeona upatikanaji wa Raisi wa Muungano nikigezogani kitakacho tumiga, ni ule ule wembe wa kunyolewa kwa udogo wa watu wake Wazanzibar kuchindwa kutoa Raisi wa Muungano Zanzibar Sisi tutaishia umakamo tu.
Tume ya Warioba imepuza tena yale maoni yakua ikiwa Mwaka huu katoka raisi wa Muungano Tanganyika Mwaka mwengine atoke Zanzibar hata kwa kigezo hicho cha chama kitakacho shinga lakini awe ni mzanzibar.
Hili kalitupilia mbali Warioba kwa kujua kua watatumia ile ile silaha yao ya wingi wa watu ili kuzibiti usawa wa Muungano na kupatikana raisi wa muungano ambae ni Mtanganyika mwenye mamuzi yote makubwa ya nchi.
Kipi kifanyike ilikua Serekali hizi 2 ya Tanganyika na Yazanzibar ipewe kila moja malaka yake kwa kutokuleta migongano ,mfano maswala ya kiuchumi kila nchi hapa inategemea mambo ya nje kukuza uchumi wake.
Swala hili litainyima Zanzibar kuchindwa kujihutumikia mambo yake ya ndani na hata kuchangia katika Serekali ya Shirikisho (Muungano) kutokana na kuchukuliwa swala hili Muunhimu kuwa la Muungano.
Zanzibar inao uwezo wa endesha Serekali yake na kuchangia serekali ya Shirikisho(Muungano) pindipo ingeweza kutolewa swala hili la mambo ya nje kusimamiwa na Serekali 2 hizi husika.
Tukumbuke kua Zanzibar haiwezi kua na matumizi makubwa yakushindwa kuweza kuchangia Serekali ya Muungano ,ispokua imefanya swala hili liwe gumu kwa makusudi kwa upande wa Zanzibar kwa kuingizwa swala la nje kwenye mambo ya Muungano.
Harama kuu za Kuchangia Muungano ni Ulinzi kama isemwavyo?
Tujue kama Zanzibar itachangia katika sehemu yake kwenye mshango wa Serekali ya shirikisho(Muungano), ni kwa pase ndogo sana kwa vile ulinzi au shuhuli nyingine za Muungano huezi kulinganisha na Tanganyika.
Tanganyika ina eneo kubwa na watu wengi kwa hio uchangiaji wake definitely utakua mkubwa ukilinganisha na Zanzibar, sasa kwa mawazo ya ulalamishi kusema Zanzibar ichangie nusu kwa nusu ,hii haiwezekani na kweli Zanzibar inaweza kushindwa,Na hili viongozi wa Tanganyika wanalijua ndio Zanzibar ikawa inapewa mgao mdogo katika misada ya nje .
Lakini ingeweza kuchangia %kubwa zanzibar bila kuyumba pindipo igeweza kuachiwa mambo ya nje yasiwe ya Muungano, na hili lililofanywa ni kukomolewa Zanzibar ishindwe kuchangia ili lengo na agenda ya Tanganyika na ccm likizi kuonekana Zanzibar inashindwa kujiweza.
Draft ya Warioba na Ndugu zake ni kuvutia zaidi maslahi upande moja wa Muungano na kuminya upande mwengine, hapa ndipo wanapo fika wakati Wananchi wa Zanzibar kukataa Muungano huu na kusema ni Ukoloni wa Tanganyika kuitawala kinguvu Zanzibar.
Na jibu la swala hili mumeliona kua Wazanzibar mauni yao tokea hapo mwanzo kabla ya kundwa rasimu hii walisema kwanza ujadiliwe Muungano kabla ya katiba ili iweze kuwatatulia utata huu wa Muungano.
Yote hayo yalipuzwa na hata maoni ya wasiotaka Muungano Warioba alichukulia hayana samani wala maana na ukitoa inaonekana umeshindwa kuchagia( work done 0).
Hii yote nikulazimishwa Wazanzibar yale watakayo wao Wakoloni wa Tanganyika, lakini wananchi wa Zanzibar kupuzwa,huu ndio ukoloni wenyewe,mpona 61% ya watanganyika walipotaka Tanganyika yao Warioba kawapa ndugu zake?.
Wazanzibar tusishurudishwe hatutaki Muungano na tuna sababu zetu.
Na kunusuru Muungano Warioba sio hivi hivi ni kurudisha tena ukoloni mambo leo,kama ni Muungano wanao ukumbadia Zanzibar ni ccm ambo wengi wa hao ni wenye asili za huko huko kwa hio hawa loose kitu hata kukiwa na mfumo wa chama kimoja.
Sisi tunawaita hawa niwalemavu wakili kwahio tuna haki wazanzibar kuwaita mentally disable na wengine huangalia shibe ya matumbo yao tu.
Kosa jengine tusije kulifanya Wazanzibar kabla hatuja ifumua Katiba yetu ya Zanzibar ya 1984.
Nilazima Baraza la Uwakilishi Zanzibar libadilishwe jina na Kuitwa Bunge la Smz la Zanzibar,Hii sio kuvunja katiba maana wao tayari watakua na Bunge lao la Tanganyika, na Katiba yao ya Tanganyika sasa ,kutakua na Wabunge wa Tanganyika kwenye Bunge lao.
Vipi sisi tusiende na Wakati kuwa na Bunge letu na wabunge wetu wa Smz ikiwa Watanganyika watakua na lao? Nilazima twende na wakati katika medali za kisiasa isiwe siku zote tunajikubalisha kujiweka nyuma hata kama ni haki yetu lakini lazima tuombe.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments