na Kissima Adolf —
RAIA yeyote wa Tanzania anaweza kumiliki ardhi kama mtu binafsi au kikundi cha watu wawili ama zaidi.
Watu hao wanaweza kumilikishwa ardhi kwa kupatiwa hati ya umiliki kwa mujibu wa sheria, kuitwaa kwa kufuata taratibu za kimila au kwa kuikalia na kuitumia ardhi kwa muda mrefu kama vile kwa miaka 12 au zaidi. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji kwa lengo la kutumia ardhi kwa uwekezaji.
Zipo aina kuu mbili za umiliki wa ardhi; umiliki wa mtu binafsi na umiliki wa pamoja.
Umiliki wa mtu binafsi
Umiliki huu unahusisha haki ya mtu binafsi kutumia ardhi akiwa na uhuru wa kufanya uamuzi binafsi bila ya kumhusisha mtu

au watu wengine.
Umiliki wa aina hii unampa mtu uhuru wa kuuza, kutoa zawadi au kuweka rehani ardhi husika bila kuomba idhini ya mtu mwingine.
Maana ya umiliki wa pamoja
Umiliki huu unahusisha haki ya mtu zaidi ya mmoja kutumia ardhi kwa pamoja.
Umiliki huu haumruhusu mtu binafsi kufanya uamuzi binafsi bila ya kumhusisha mwenzake au wenzake.
Uamuzi utakaofanywa na mtu mmoja bila ya kumhusisha mwenzake au wenzake juu ya kuuza, kutoa zawadi au kuweka rehani ardhi husika unakuwa batili.
Ieleweke kwamba kila mmilikaji wa pamoja atapewa hati yake ya umilikaji wa ardhi wa pamoja.
Kwa hiyo kila mmilikaji wa pamoja awe mwanamke au mwanamume ahakikishe kuwa anapata hati ya umilikaji.
Wanawake wanaomiliki ardhi pamoja na wanaume (kwa wanandoa) wahakikishe kwamba kila mmoja wao anapata hati ya umilikaji.
Umiliki wa pamoja nao upo wa aina mbili kama vile umiliki wa pamoja wa mafungu yasiyogawanyika na umiliki wa pamoja wa mafungu yanayogawanyika.
Umiliki huu utawahusu wanandoa tu, wakipenda, kwa wengine lazima kwanza kipatikane kibali cha mahakama.
Wamiliki, wanamiliki ardhi yote kwa ujumla, umiliki wa aina hii huandikishwa kwa msajili wa hati ya umiliki wa ardhi.
Utoaji wa ardhi au ubadilishaji wa umiliki, hufanyika kwa kibali cha wamiliki wote.
Utoaji wa ardhi ni lazima ufanyike kwa makubaliano ya wamiliki wote pale inapotokea kifo cha mmiliki mmojawapo, fungu lake hutambuliwa kama sehemu ya mali zake linaweza kurithiwa na warithi wake.
Mmoja wa wamiliki akifa masilahi yake yote yatarithiwa na mmiliki au wamiliki waliobaki. Umiliki huu pia huandikishwa kwa msajili.
Umiliki wa pamoja baina ya wanandoa
Umiliki wa ardhi wa pamoja unawezekana kabisa.
Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 inaeleza kuwa wanandoa (mke na mume) wanaweza kumiliki ardhi katika mafungu yanayogawanyika au katika mafungu yasiyogawanyika.
Hapa ieleweke pia kwamba kama mwanandoa mmoja anamiliki ardhi kwa jina lake pekee lakini baadaye mwanandoa mwenzake akachangia katika kuiendeleza ardhi hiyo, mwanandoa yule aliyechangia atakuwa amepata haki ya kumiliki ile ardhi kwa hisa (share) zisizogawanyika wakichangia umilikaji huo na yule mwanandoa aliyepewa kwanza haki ya kumiliki ardhi.
Utaratibu huu ni mzuri na unawahakikishia wanawake haki yao ya kumiliki ardhi ukilinganisha na sheria za mirathi za kimila zinazowanyima wanawake haki yao ya kurithi ardhi ikiwa ni njia mojawapo ya kupata na kumiliki ardhi.
Faida za kuwa na hati ya kumiliki ardhi
Ukiwa na hati au cheti cha kumiliki ardhi una uhakika wa usalama wa ardhi yako unayomiliki, nyumba au maendeleo yoyote uliyoyafanya katika ardhi hiyo.
Hati au cheti kinaweza kutumika katika kuomba mkopo benki ikitumika kama rehani.
Hati au cheti kinaweza kutumika kama dhamana mahakamani na polisi. Hati au cheti kinasaidia kuhamisha umiliki wa ardhi kiuhalali na kwa uhakika.
Baada ya kuangalia maana ya umiliki wa mtu binafsi, umiliki wa ardhi kwa wanandoa na umiliki wa pamoja, pamoja na faida za kumiliki hati ya ardhi ni vema tukavijua vyombo ambavyo kisheria vimepewa mamlaka ya kutatua migogoro ya ardhi.
Kwa mujibu wa sheria, tukianza na maeneo ya vijijini, kila kijiji ni lazima kiwe na na baraza la ardhi la kijiji.
Ili uamuzi wa baraza hili utambulike kisheria ni lazima muundo wa baraza hili likidhi matakwa ya sheria.
Usimamizi wa mabaraza
Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji yatakuwa chini ya usimamizi wa Msajili wa Vijiji.
Kazi ya usimamizi inajumuisha uendeshaji wa haya mabaraza akisaidiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri husika.
Uendeshaji ni kwa maana ya matumizi na mapato. Mkurugenzi anatakiwa wakati wote kuhakikisha kuwepo kwa mabaraza haya katika ngazi ya vijiji vyote vilivyosajiliwa.
Uwasilishaji wa malalamiko
Mtu yeyote mwenye malalamiko kuhusu mgogoro wa ardhi, anaweza kuyawasilisha kwa njia ya maandishi au kwa njia ya mdomo, kwa Katibu wa Baraza la Ardhi la Kijiji na yeye atayawasilisha kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Kijiji.
Kama malalamiko yatatolewa kwa mdomo, basi Katibu wa Baraza la Ardhi la Kijiji atayanakili na kuwasilisha nukuu hiyo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kijiji.
Kanuni za uendeshaji wa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji
Baada ya wajumbe wa Baraza la Ardhi la Kijiji kuchaguliwa, watamchagua Mwenyekiti na Katibu wa Baraza.
Mwenyekiti ndiye atakayekuwa kiongozi wa Baraza, na ndiye atakayewajibika kutoa uamuzi mbalimbali wa kijiji.
Baada ya kusuluhisha mgogoro, Baraza la Ardhi la Kijiji linapaswa kuandika muhtasari wa kikao hicho, wasuluhishi, pamoja na wadawa wengine.
Wenye mgogoro wanapaswa kutia sahihi zao na waondoke na nakala ya uamuzi. Wajumbe wa Baraza watafanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kama hicho kama bado wanazo sifa za kuendelea kuteuliwa kwa nafasi hiyo.
Mjumbe hataruhusiwa kusuluhisha mgogoro wowote unaomhusu au unaoihusu familia yake au hata jamaa yake, kwa sababu ya mgongano wa kimasilahi.
Wadau wa mgogoro wanaweza kuamua kusuluhishwa katika shauri lao na Baraza la Ardhi la Kijiji au kwenda moja kwa moja kwenye Baraza la kata.
Baraza la Ardhi la Kijiji halina uwezo kusuluhisha au kusikiliza mgogoro kama thamani ya mali inayolalamikiwa itakuwa katika ardhi iliyopimwa katika mipango miji.
Kukata rufaa au kuhamisha mgogoro
Sheria ya Ardhi ya Kijiji ya Mwaka 1999 na ile ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi inatoa mwanya kwa wadau katika mgogoro husika kuchagua mahali pa kusuluhisha au kusikilizwa shauri lao.
Hata hivyo, wadau wanashauriwa kuanza na Baraza la Ardhi la kijiji kabla ya kwenda Baraza la Kata.
Kwa upande mwingine Sheria ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi inatoa mwanya wa kukata rufaa endapo upande wowote katika mgogoro hautaridhika na usuluhishi wa Baraza la Ardhi la Kijiji.
Upande usioridhika utapeleka mgogoro huo katika Baraza la Ardhi la Kata. Hata hivyo ikitokea kuna upande ambao bado haujaridhika na uamuzi uliotolewa na Baraza la Ardhi la Kata, bado wanaweza kukata rufaa kwenda kwenye Baraza la Nyumba la Wilaya.
Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya
Kwa mujibu wa Sheria za Ardhi, hasa Sheria ya Ardhi ya Mjini pamoja na Sheria ya Ardhi ya Vijiji ( Land Act No 4 and Village Land Act No 5) kila wilaya, mkoa kutakuwepo na baraza la ardhi kadri itakavyowezekana, na baraza hilo litaitwa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.
Na baraza hili la wilaya litafanya majukumu yake yaliyomo ndani ya wilaya au mkoa na si vinginevyo kama itakavyokuwa imeelekezwa.
Katika kusikiliza mashauri ya aridhi, baraza hili litakuwa limekamilika kisheria endapo kutakuwapo na mwenyekiti pamoja na wazee wa baraza wasiopungua wawili.
Wazee hawa wa baraza watahitajika kutoa mawazo yao katika shauri husika kabla mwenyekiti hajatoa uamuzi katika shauri husika.
Na ili kufikia uamuzi mara nyingi mwenyekiti atalazimika kufuata ushauri au maoni ya wazee wa baraza lakini mwenyekiti halazimishwi kufuata mawazo hayo, cha msingi anaweza kuyakataa kwa kutoa sababu itakayoonesha kwanini anapingana na mawazo ya wazee wa baraza.
Kwa kawaida mwenyekiti katika Baraza la Ardhi la Wilaya huchaguliwa na waziri husika. Mwenyekiti lazima awe na taaluma ya sheria na ataweza kuifanya kazi yake hiyo kwa muda wa miaka mitatu.
Vilevile ataweza kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo. Kwa mujibu wa sheria, mwenyekiti huyo kabla hajaanza kazi yake ni lazima ale kiapo kitakachosimamiwa na mkuu wa mkoa lilipo baraza.
Waziri wa Ardhi baada ya kujadiliana na mkuu wa mkoa atachagua wazee wa Baraza la Ardhi la Wilaya wasiopungua saba, kati yao wakiwemo wanawake watatu.
Mtu yeyote mwenye umri kuanzia miaka 21 ataweza kuchaguliwa kuwa mzee wa Baraza la Ardhi la Wilaya. Isipokuwa mtu hawezi kuteuliwa kama mzee wa baraza endapo tu, si mkazi wa kila siku katika wilaya husika, mtu huyo hawezi kuteuliwa kama ni mbunge au akili yake si timamu au mtu huyo alishawahi kufungwa au si raia wa Tanzania.
Mwenendo wa shauri katika Baraza la Ardhi la Wilaya linapaswa kusikilizwa sehemu ya wazi ili kuruhusu umma kufika na kuangalia mwenendo mzima wa shauri.
Mlalamikaji au mlalamikiwa anaweza kufika kwenye baraza na kusimama yeye binafsi au kwa kutumia wakili wake au kwa kutumia ndugu yake.
Katika usikilizaji wa mashauri, Baraza la Ardhi la wilaya litaweza kutumia lugha ya Kiingereza au Kiswahili kutegemea na mwenyekiti atakavyoamua, akizingatia hali halisi ya shauri lililopo mbele yake.
Lakini maandishi pamoja na hukumu lazima viwekwe kwa lugha ya Kiingereza.
Wasiliana na mwandishi kupitia: 0713 401812 adolfkissima@yahoo.com

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments