THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
Kanuni za Msingi za Chama (Kwa mujibu wa KATIBA YA CHAMA)
KANUNI:
Ili Chama kiweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na nidhamu, ni wajibu wa Chama kutengeneza Kanuni zitakazohusu wanachama, mwenendo wa viongozi, hifadhi na udhibiti wa mali za Chama zitakazopitishwa na Baraza Kuu la Taifa la Chama.
UANACHAMA:
1. Uanachama utakuwa wa mtu mmoja mmoja binafsi.
2. Raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwenye umri wa miaka kumi na nane na mwenye akili timamu atakayeomba kuwa mwanachama, atajaza fomu ya maombi na kuirejesha kwenye tawi.
3. Mwananchi aliyekubaliwa kuwa mwanachama atalipa kiingilio na ada ya kila mwezi kama zitakavyopangwa na Baraza Kuu la Taifa la Chama.
4. Mwanachama anaweza kujilipia kwa jumla kila mwaka au mwezi hadi mwezi.
5. Mwanachama atakabidhiwa kadi yake na Mwenyekiti wa Chama mbele ya Katibu wa Tawi na Mjumbe mmoja wa kamati ya Tawi.
NIDHAMU YA CHAMA:
1. Kwa madhumuni ya kuhakikisha nidhamu ya Chama na bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mwanachama atazingatia kwa ukamilifu misingi ya nidhamu kwa mujibu wa katiba ya Chama.
2. Endapo utatokea mgongano wa wanachama kwa wanachama, utadhibitiwa na kanuni za Chama kwa mujibu wa uzito wa kosa lilivyo katika ngazi ya Chama inayohusika.
3. Ikiwa mwanachama hakuridhika na uamuzi wa ngazi yake anayo haki ya kuomba rufaa katika ngazi ya juu mpaka Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama.
4. Mwanachama atakayepoteza sifa za uanachama atarudisha kadi yake ya uanachama katika Tawi.
5. Mwanachama mwadilifu takuwa yule anayeheshimu Katiba, anayefuata kanuni, anayelipa ada zake kwa wakati na anayehudhuria vikao vya Chama vinavyomhusu.
6. Mwanachama asiyelipa ada yake kwa muda wa miezi 12, au asiyehudhuria vikao vya Chama vinavyomhusu kwa muda wa mwaka mzima bila udhuru atakuwa amejiachisha mwenyewe uanachama.
UONGOZI NA MAADILI:
1. Iwapo kiogozi wa Chama ameshindwa kutekeleza wajibu wake wa uogozi wa ngazi yake aliyokabidhhiwa, ataonywa na kiongozi mkuu wa ngazi yake, au na uongozi wa Kamati ya ngazi yake, kwa maandishi baada ya kusikilizwa Taarifa ya hatua hiyo itafikishwa ngazi ya juu.
2. Kwa kosa la pili na la tatu Kiongozi atakaripiwa na kamati ya uongozi ya ngazi yake.
3. Kwa kosa linalofuata, atafikishwa ngazi ya juu pamoja na taarifa zake zote kwa maamuzi ya mwisho.
4. Iwapo Mwenyekiti au Katibu wa ngazi inayohusika anahusika na mgogoro, uongozi wa ngazi hiyo, mkutano huo utasaididwa na mjumbe mmoja au wawili kutoka ngazi za juu za Chama, kutafuta ufumbuzi kwa mujibu wa utaratibu wa kanuni hizi.
TARATIBU ZA MCHUJO WA UONGOZI:
1. Katika uchaguzi wa chama wa ngazi yoyote, kila mwanachama anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika Chama. Vikao vya uchaguzi vitakuwa na taratibu za kuchuja mgombea uongozi.
2. Endapo wagombea watakuwa wengi, Mkutano wa uchaguzi unaohusika, utasimamisha wagombea wote kwa pamoja kugombea nafasi inayohusika.
3. Wagombea wote watapigiwa kura, na yule (wale) atakayepata kura ying zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya kura zote zilizopigwa atakuwa kiongozi wa ngazi hiyo.
4. Kwa wale wanaogombea nafasi za juu ya ngazi yao, kutakuwa na utaratibu wa kuchuja mpaka kufikia Mkutano Mkuu unaohusika.
5. Waombaji wawili waliopata asilimia kubwa ya kura kuliko wagombea wengine wote watapelekwa ngazi ya juu kwa kila nafasi ya kuchaguliwa. Wagombea watatolewa wawili, isipokuwa kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Manaibu wa Katibu Mkuu – wa Taifa, na wagombea Urais, watatolewa wagombea watatu. Mkutano Mkuu wa Taifa utawachuja wagombea hao na kupatikana mmoja wao ambae ataungana na wagombea wa Vyama vingine, ikiwa ni uchaguzi wa Serikali.
HIFADHI NA UDHIBITI WA MALI YA CHAMA:
1. Chama kitakuwa na njia za kujipatia fedha za matumizi na mali kwa njia zifuatazo:
a) Michango ya uanachama
b) Ruzuku kutoka kwa wanachama, wafadhili na wahisani wa ndani na njeya nchi, na ruzuku kutoka serikalini.
c) Mapato kutoka miradi mbalimbali ya uchumi kama vile viwanda, mashirika na makampuni.
d) Chama kitajipatia mapato kutokana na shughuli maalum za kijamiii na burudani.
Shughuli zote za mapato na mali zitasimamiwa na Bodi ya Wadhamini.
2. Udhibiti wa mali za Chama
a) Mkurugenzi wa Kitengo cha Fedha anawajibika kuweka madaftari ya mali na vitabu vya fedha, kwa mujibu wa sheria za nchi, akishirikiana na Bodi ya Wadhamini.
b) Mali isiyoondosheka ya Chama itaorodheswa na kuhifadhiwa ndani ya DAFTARI YA MALI YA CHAMA (Register Book)
c) Mapato na matumizi ya fedha ya Chama yatafanywa kwa mujibu wa stakabadhi rasmi za Chama.
d) Ukaguzi wa mali na fedha za Chama utafanywa na makampuni yaliyosajiliwa nchini kwa mujibu wa sheria.
e) Mali zote za Chama zinazoondosheka zitahifadhiwa na Mhakiki mali (Verifier) wa Chama.
f) Fedha zote za Chama zitawekwa BENKI YA TAIFA YA BIASHARA na BENKI YA ZANZIBAR.
g) Kiengo cha Fedha kitatuna Kanuni ndogondogo za kudhibiti matumizi ya kila siku ya fedha chini ya idara ndogo ya UDHIBITI WA NDANI WA FEDHA>
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments