Ndugu zangu.
KUNA miongoni mwetu tumemsoma mwanafasihi Shaaban Robert. Kuna mahali kwenye kitabu chake ' Kusadikika', Shabaan Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.
Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.
Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.
Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.
" Nafikiri, ndio maana naishi"- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.
Na maarifa ya Sayansi yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.
Mengine yanayotokea katika jamii ni ya dhahiri kabisa. Ni ukweli. Na jambo la kweli hata likifanyiwa hila, basi, hatimaye hila hushindwa.
Maana, hila na ghilba huuchelewesha tu ukweli kuweza kudhihiri, lakini, kamwe haviwezi kuuzuia.
Ni Neno La Leo.
Maggid.
http://mjengwablog.comKUNA miongoni mwetu tumemsoma mwanafasihi Shaaban Robert. Kuna mahali kwenye kitabu chake ' Kusadikika', Shabaan Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.
Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.
Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.
Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.
" Nafikiri, ndio maana naishi"- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.
Na maarifa ya Sayansi yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.
Mengine yanayotokea katika jamii ni ya dhahiri kabisa. Ni ukweli. Na jambo la kweli hata likifanyiwa hila, basi, hatimaye hila hushindwa.
Maana, hila na ghilba huuchelewesha tu ukweli kuweza kudhihiri, lakini, kamwe haviwezi kuuzuia.
Ni Neno La Leo.
Maggid.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments