[wanabidii] Tahadhari kwa Taifa

Tuesday, August 20, 2013

Kuwa na jeshi kubwa, vifaa vya kisasa,na mbinu za hali ya juu kijeshi  hakutoi uhakika wa kushinda vita.
     Naanza kuwasilisha, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu hali ya mambo inavyoendelea ndani na nje ya mipaka yetu ndilo lililonisukuma kuandika haya. Kwa nini nimeanza na msemo huo, nimegundua kama Taifa tumejisahau tunaamini sana nguvu za majeshi yetu, ambavyo ni sawa kabisa, wengine wamekwenda mbali zaidi wakirejea ushindi dhidi ya. Nduli Ammin lakini napenda kuwakumbusha Kuwa vita ile hatukushinda kwa Kuwa na jeshi bora tu bali umoja na mshikamano wetu ulikuwa chachu nyingine ya ushindi ule. Leo hii kama Taifa tumekosa hayo yote kuanzia serikalini hadi uraiani, Naamini mbinu aliyoamua kuitumia Paul Kagame ni kutokana nakuona udhaifu moja kwenye serikali yetu, leo si ajabu kuwa na kauli zinazokinzana juu ya jambo moja ndani ya serikali na vyombo vyake, simaanishi ni vibaya kutoa mawazo tafauti ila kwa viongozi walipaswa kuwa wanamalizana wao kwa wao kwetu waje na kauli moja, inayoonyesha msimamo wao kama viongozi. Pili kama jamii hatuna umoja tena kama ulioasisiwa na Malimu Nyerere, leo tunachinjana, tunamwagiana tindikali, tunachomeana nyumba za Ibada huko ni kuonyesha umoja na mshikamano wetu uko katika majaribu makubwa. Tukumbuke wakoloni kabla hawajatutawala walihakikisha wanatugawa iliitwa "devide and rule ",sasa sisi leo hatujagawanywa ila tumejigawa wenyewe hapo tunampa adui nafasi ya kutushinda kirahisi, maana hata wanajeshi na polisi hawana uhakika na usalama wao na familia zao watawezaje kuhakikisha usalama kwenye Taifa? Umoja wa kisovieti ulishindwa kwenye vita baridi na Marekani na washirika wake baada ya kuhakikisha wamewagawa kwanza. Ni rai yangu kwa serikali na viongozi wetu kuhakikisha wanatengeneza Umoja wa kitaifa kwa kuhakikisha wanasimamia sheria na haki huku wakipinga unyonyaji na dhuluma kwa nguvu zote bila kujali aliyefanya wala kufanyiwa. Pili serikali iwe na umoja katika misimamo yake mbalimbali na si kuruhusu mkanganyiko wa misimamo baina yao. Tukumbuke sikuhizi moja ya mbinu kuu za kijeshi ni kuhakikisha kunakuwa na "internal disruption" kwa adui ndicho alichofanya Marekani Iraq, akaweza kumng'oa Saadam na ndicho anachojaribu kufanya sasa Korea ya kaskazini, kwa kuwawekea vikwazo ili waichukie serikali yao. Udhaifu inayoonyesha sasa kwenye serikali na jamii yetu juu ya umoja na mshikamano wetu utatufanya tupigwe hata na mataifa madogo kama Rwanda kwa kuwa tumekosa umoja, Tukumbuke kuwa "Umoja ni Nguvu Utengano ni Udhaifu" Mkristo na Muislam wote tu Watanzania, Mgogo Mnyiramba wote tu Watanzania, tuipende, tuijali, tuiheshimu na kuilinda Nchi yetu na yeyote asiyetutakia mema . Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments