[wanabidii] CCM-Kagera yawafukuza Madiwani 8 wa manispaa ya Mji wa Bukoba

Wednesday, August 14, 2013
Katibu wa CCM mkoa amemaliza press conference hi vi punde na kufafanua kuwa Halmashauri Kuu ya Mkoa imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani nane wa manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutwa nyadhifa zao za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

Majina ya madiwani hao nane waliofukuzwa ni haya yafuatayo:-
  1. Richard Gaspar (Miembeni )

  2. Murungi Kichwabuta (Viti maalum)

  3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

  4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

  5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

  6. Robert Katunzi (Hamugembe)

  7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

  8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo)

Matias Byabato, Chanel TEN, Bukoba --- (BukobaWadau blog)

------------

Taarifa iliyotolewa na  Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera Avelin Mushi, imesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.

Mushi amesema kuwa  kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya Mbunge na Meya ambapo Rais Kikwete akiwa ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kutoendelea na mgogoro huo lakini maagizo  hayo yalipuuzwa.

Pia, amesema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini wahusika wote wamekuwa wakikahidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao. (CCM Chama blog)


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/ccm-kagera-yawafukuza-madiwani-8-wa-manispaa-ya-mji-wa-bukoba.html#ixzz2bvok7b86

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments