[wanabidii] INGETREX TANZANIA 2014-NAWAKARIBISHA DIAMOND JUBILEE!

Friday, May 16, 2014
Wanabidii,

Nawakaribisha Ingetrex Tanzania, ni Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, ambayo yatafanyika kwa siku 3 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, kuanzia Tarehe 15 hadi 17 ya mwezi huu wa May.

Katika maonyesho hayo, makampuni mbalimbali kitaifa na kimataifa, yataonyesha bidhaa zake, ila pia waandalizi wa Maonyesho hayo, wametoa fursa mahsusi kwa makampuni na wajasiliamali wadogo na wa kati wa Kitanzania wenye bidhaa za viwango vya kimataifa, kuja kuonyesha bidhaa zao.
 
Kwa maelezo zaidi, tembelea hapa INGETREX TANZANIA | Dar es Salaam / Tanzania.

 
Kwa Wanabidii mlioko Dar, na hasa wale wenye nafasi, karibuni sana Diamond Jubilee leo na kesho, kuja kuona kitu kinachoitwa International Quality Products na kujiuliza kama na sisi Tanzania tutakuja kuanzisha viwanda na kuzalisha bidhaa za viwango hivyo vya kimataifa, au tutaendelea lifanywa ni masoko tuu ya bidhaa za wenzetu?!.

Kwa taarifa tuu, kwa msiojua, hata toothpicks tunazotumia, tumeshindwa kutengeneza, tunaagiza kutoka nje!.
Hapo sijazungumzia pini, vwembe, vifungo, miswaki, etc etc, hivi ni vitu vidogo vidogo tuu, tunashindwa!, kwa vikubwa jee?!.
 
Natanguliza shukrani.

Pascal.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments