PROF WAMBA – AFRIKA IWE NA CHOMBO KIMOJA CHA KUSIMAMIA MAJI
Kama mnavyojua tulikuwa na mkutano wa prof wamba uliojadili masuala mbalimbali moja wapo ni hili la maji ya Mto Nile kati ya Misri na nchi nyingine zinazotumia mto huo au maji ya kwenye mto pia suala la ziwa nyasa kwa ufupi kabisa .
Katika suala la maji kwa ujumla yeye anasema anapenda kuona afrika ikiwa moja katika kutetea matumizi ya maji na kwamba umoja wa afrika iwe na nguvu na uunde chombo kimoja cha kusimamia maji yote kwa maslahi ya mataifa yote ya afrika kuliko ilivyosasa ambapo baadhi ya mataifa yamejiundia vyombo vyao kama nile basin ,Tanganyika basin na nyingine nyingi .
Kukatolewa msisitizo kwamba sasa hivi baadhi ya maeneo yanaishiwa maji kama CHAD na NIGER haya maeneo yanahitaji maji kwa ajili ya uhai , vile vile kina kinavyozidi kupungua katika mto nile inaweka rehani maisha ya watu wa misri na mataifa mengine yanayotumia maji uhai wao .
Utaona kwa mfano CHAD na NIGER hawana maji lakini wana URANI na madini mengine yanayoweza kuzalisha umeme ambao unaweza kusafirishwa kupelekwa maeneo mengine ambayo nayo yanaweza kutoa maji bila kutumia maji hayo kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa mara nyingine .
Mfano mwingine uko kwenye nchi ya Kongo DRC wale wana maji mengi na kwa siku za karibuni wamekuwa na mpango wa kuuza kwa nchi nyingine kama Botswana na Namibia kwa ajili ya matumizi pia kongo ina madini na inaweza kuzalisha umeme kwa kiasi kikubwa cha kutosheleza afrika nzima .
mimi binafsi nimependa hili wazo la kuwa na chombo kimoja cha kusimamia masuala ya maji afrika nzima chombo hichi kinaweza kuwahikikishia amani na utulivu unaohusu maji mamilioni ya waafrika na nchi zao .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments