[wanabidii] Mabaya haya ni yetu sote

Friday, July 19, 2013
Salaam kwa wote!
Maadili yanafundishwa kwenye dini na hata mashuleni.Maadili haya haya yakipotoshwa au yasipofatwa ndio huleta uharibifu wa watoto mpaka watu wazima maofisini.

Maadili mazuri yanaanzia kwako,kwa jirani,mtaani na hadi kazini.Mambo mengine huwa tunalaumu watu Fulani au dini Fulani bila kujilaumu wenyewe kwanza na kuangalia je mimi Nina maadili.

Utakuta Kuna vijana hawaendi shule na wewe unawajua kwakuwa wanashinda mtaani kwako wakicheza kamali lakini wewe unanyamaza eti kwakuwa sio wa kwako hayo sio maadili mazuri na ndio inapelekea kulaumu walimu wakati wewe uwezo unao wa hata kuwafukuza tuu na kuwaambia waende shule.
Maadili mema ni kuwa na mfumo mwema wa maisha unaweza kuruhusu kukataza mambo yanayoathiri jamii na sio kutugemea watu fulani.

Dereva wa daladala anatukana ovyo wakati ndani ya daladala mmekaa watu wa rika tofauti kwanini wewe usikemee na kukaa na kuangalia tuu.

Mambo mengi yanatokea katika jamii yetu na sisi tukiyashuhudia na bila kuchukua hatu yoyote ambayo ipo ndani ya uwezo Wako.
Tubadilike basi na si kukaa kimya tuu bali tukemee na kukaakulaumu serikali wakati uwezo tunao wa kurebisha matatizo katika jamii yetu.

Wazungu wanamsemo wao wanasema "mabadiliko ni wewe,mabadiliko ni sisi".
Basi tuwe waafrika ambao tunaamini watoto hulelewa na jamii nazi na mzazi pekee yk au mwalimu tuu.

Sio mwandishi mzuri lakini najitahidi kusema ninayo yaona mimi,kama nimekosea tusameane.

Sent from my Windows Phone

Share this :

Related Posts

0 Comments