Ndugu zangu,
Leo mchana niliingia na kulikuta gari hilo pale nyumba ya Makumbusho Dar. Itakumbukwa, kuwa Mandela alifika kwa Julius Nyerere Msasani mwaka 1962. Alishangazwa sana kumwona Rais wa nchi anaendesha mwenyewe gari ya kawaida kabisa aina ya Austin( Pichani).
Utotoni kila sikukuu tulikuwa na mazoea ya
-- Leo mchana niliingia na kulikuta gari hilo pale nyumba ya Makumbusho Dar. Itakumbukwa, kuwa Mandela alifika kwa Julius Nyerere Msasani mwaka 1962. Alishangazwa sana kumwona Rais wa nchi anaendesha mwenyewe gari ya kawaida kabisa aina ya Austin( Pichani).
Utotoni kila sikukuu tulikuwa na mazoea ya
kwenda Makumbusho, Magogoni na tulihitimisha kwa kupanda pantoni kwenda ng'ambo ya pili ya bahari; Kigamboni. Hapo ndio siku kuu imekamilika.
Nilipenda sana kuingia Makumbusho ya Taifa. Moja ya sehemu niliyoipenda sana ni kuangalia picha za kumbukumbu ya Dar es Salaam tangu ikiitwa Mzizima. Picha hizo sasa hazipo.
Lakini, nilipenda pia kuangalia magari yaliyotumika na viongozi zamani. Nakumbuka miaka hiyo niliiona Austin hiyo ya Nyerere pichani kuwa bado ilikuwa gari ya maana sana, tena kubwa!
Leo najiuliza, hivi Julius Nyerere, mkewe na watoto walitosha kweli kwenye kigari hicho, au labda walipakatana!
Naam, historia ni mwalimu mzuri.
Maggid,
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments