[wanabidii] PINGAMIZI LA CHADEMA DHIDI YA MGOMBEA WA CCM JIMBO LA KALENGA LATUPILIWA MBALI

Thursday, February 20, 2014
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalenga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Iringa vijijini Pudensiana Kisaka.
 Godfrey Mgimwa; Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM

PINGAMIZI lililowekwa na Mgombea wa  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Tendega dhidi ya Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Godfrey Mgimwa limetupiliwa mbali.
 Mgimwa amewekewa pingamizi hilo kwamba sio raia wa Tanzania na kwamba watu waliomdhamini hawatokei jimbo la Kalenga.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kalenga, Pudensiana Kisaka alisema tume hiyo iliamua kuruhusu kampeni ziendelee baada ya upande wa walalamika kujishindwa kupeleka vielelezo.

Alisema baada ya kupata pingamizi hilo, tume iliagiza pande zote mbili, kupeleka vielelezo vyake ili kujiridhisha na pingamizi hilo.
Hata hivyo chadema, walishindwa kupeleka uthibitisho wa pingamizi lao kwa muda ulipangwa na badala yake, walipeleka barua ya kusisitiza pingamizi hilo.

Katibu wa CCM, wilayani Iringa Amina Imbo alisema mgombea wake ni raia wa kuzaliwa wa Tanzania na kwamba, pingamizi hilo halina maana na kamwe halitaweza kuvuruga kampeni za chama hicho.

Imbo aliongeza kuwa CCM ilisimamia kikamilifu kuhakikisha, fomu za mgombea zidhaminiwa na wananchi wa jimbo husika ambao waliambatanisha shahada za kupigia kura kutoka jimboni na si vinginevyo.

Mgimwa amezaliwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa, amesoma shule ya msingi wilolesi na baadae kujiunga na shule ya sekondari ya Njombe (NJOSS), kabla ya kwenda jijini na Dar es salaan kisha nchini uingereza kwa masomo yake ya elimu ya juu.

Anayo passport ya kusafiria inayoonyesha kwamba ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa na  cheti cha kuzaliwa na hajawahi kukataa utanzania.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments