Ndugu zangu,
Nahofia, kuwa Watanzania tumejikita kwenye ndoto ya utajiri wa gesi na mafuta. Hivyo, kusahau kilimo chetu. Hiyo ni hatari kwa uchumi wetu.
Tunafikiria utajiri wa gesi na mafuta kana kwamba katika dunia hii ni sisi tu Watanzania ndio wenye utajiri wa akiba ya gesi na mafuta. Hatujui, kuwa katika dunia hii kuna nchi zilizo na akiba hizo za mafuta na gesi lakini bado uchumi wao hauwafanyi watu wao wawe ni wenye neema tu.
Nao wanafikiria pia kwenye vyanzo vingine vya kuinua uchumi wao ikiwamo kilimo. Na ukweli tunaoishi nao sasa ni huu, kuwa gesi na mafuta bado havijawa uti wa mgongo wa taifa letu. Kilimo kimekuwa na huenda kitabaki kuwa UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU. Na ndio UHAI WETU.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments