Ndugu zangu,
Mwaka jana nilikimbia na kumaliza mbio za kilomita 21 kwa muda wa heshima kabisa, chini ya saa mbili. Ni Ruaha Marathon hapa Iringa.
Na kesho Jumamosi kuna Ruaha Marathon ya pili. Sitakimbia. Maana, Afrika usiianze safari kabla ya kuupima upepo wa safari yenyewe.
Kila jambo na maandalizi. Katika miezi ya karibuni ratiba zangu za jogging zimevurugika kiasi. Hivyo, siko kwenye physical form ya kawaida yangu. Na kilomita 21 ni kilomita 21. Ni sawa na kutoka Ubungo hadi Kibamba. Ukizilazimisha unaweza kuzimaliza kwa kubebwa kwenye machela, kama zipo!
Naam, kwa mwanadamu muhimu ni kutambua, kuwa kwa kila jambo unalotaka kutenda, basi, jitahidi kufanya maandalizi. Na maandalizi yasifanywe siku ya tukio lenyewe.
Vinginevyo itakuwa sawa na kisa cha bwana aliyeshtuka siku ya mnada na kuamua kumlisha ng'ombe wangu majani mengi ili aongezeke kilo!
Na Wahenga walisema; ng'ombe hanenepi siku ya mnada!
Nawatakia Marathon njema wote watakaokimbia hiyo kesho.
Maggid,
Iringa
0754 678 252
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments