Alipanda juu, juu ya mkuyu
Yesu akamwiita, Zakayoo Njoo
Zakaayo Njoo, Shuka juu ya mti...!"
Ndugu zangu,
Wimbo huo wa kwaya niliusikia utotoni mwangu. Nilijiuliza sana kuhusu kisa cha Zakayo na Bwana Yesu.
Hakika kinahusu hesabu pia, kama tulivyoona utata wa ushahidi wa Kalumekenge na Bwana Njau juu ya urefu wa mtuhumiwa. Njau alimwona mtuhumiwa mfupi kwa vile yeye ni mrefu, na Kalumekenge alimwona mtuhumiwa mrefu kwa vile yeye ni mfupi.
Kwenye Biblia inaandikwa, kuwa Zakayo alikuwa mkusanya kodi. Alikuwa dhalimu kwa watu. Aliwanyanyasa katika kukusanya kwake kodi.
Siku Bwana Yesu alipofika kwenye mji wao, umati wa watu ulikusanyika. Zakayo naye alitaka kumwona Yesu. Kwa vile alikuwa mfupi, alipanda juu ya mti wa Mkuyu.
Yesu akamwona. Akamwita; Ewe Zakayo, shuka juu ya mti...!
Yesu akaenda hadi nyumbani kwa Zakayo. Tendo hilo lilimstaajabisha Zakayo. Wanazuoni wa Kikristo huenda wanaweza kukifafanua zaidi kisa hiki .
Lakini, tukirudi kwenye lile la hesabu. Yumkini Zakayo alipokuwa juu ya mti kwake Yesu alikuwa ni mtu mfupi. Na mara Yesu alipomsogelea Zakayo, bai, Yesu akawa mrefu!
Ni Neno Fupi La Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
http://mjengwablog.co.tz/ --
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments