[wanabidii] Ridhiwani Kikwete : SINA UHUSIANO NA TANZANIA LOAN SOCIETY

Friday, February 08, 2013
Habari zenu, mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na
wale wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine
mtakapo soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili
kuweka hali vizuri .

maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi
kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine
mambo yangu yatanyooka.hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika
ufanikiwe. lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu,
kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya
dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.

hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata twitts juu ya
kitu kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au
nyengine kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya
Raisi Barack Obama kuja tanzania kupitia Raisi Dr. Jakaya Kikwete na
sasa mie nikishirikiana na Waziri Mkuu Bwana Mizengo Kayanza Pinda
tunauendesha.Jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba tumia
nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa watanzania na wale wote
ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye
kurasa hii.

kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI
SI LA KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa
hela yake basi atakuwa AMETAPELIWA.

kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania
kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao. maana wanaotangaza vitu
kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU
ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au
kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.

Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa
mliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona
pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla
hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.

Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine
wamekuwa wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe
mfupi wa maneno pia. pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au
nyengine wameathiriwa na zoezi hili. lakini haukuwa nia yangu kuona
dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa
uchunguzi wa kina lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka
maana unaweza fanya jambo kumbe ndiyo unalikuza. lakini pia niwaombe
wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za face book
zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli waone jinsi gani
wanaweza kulizungumzia jambo hili ili kuwasaidia wengi ambao
wameathirika na imani yao juu ya hili

MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE
AKHSANTENI KWA KUSOMA TAARIFA HII.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments