[wanabidii] CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA

Friday, February 08, 2013
TANZANIA MEN'S RIGHTS ASSOCIATION
CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA

"TAMRA"
Equal treatments for all
UTANGULIZI

TAMRA ni Asasi ya kiraia iliyoanzishwa na wanaume wa Tanzania kwa
lengo la kutoa msaada wa Kisheria pamoja na Elimu ya Haki na Wajibu
katika mahusiano ya kindoa kati ya mwanamke na mwanaume.
Kuanzishwa kwa asasi hii kumekuja katika kipindi hiki baada ya tafiti
mbalimbali kuonyesha kuwa wapo wanaume wengi wanaofanyiwa vitendo vya
ukatili katika masuala ya ndoa kwa kunyimwa haki zao za kindoa
kutupiwa virago pindi mwanamke anapoamua kumchoka mwanamme kufuatana
na kukosa kipato, kupungukiwa nguvu za kiume na mambo kama hayo ,
jambo ambalo limeonekana kuwa ni chanzo cha migogoro katika ndoa
inayosababisha ongezeko la watoto wanaoishi bila wazazi wa pande zote
mbili yaani [ Baba na Mama] huku hali hii ikiigharimu jamii na
wanandoa kupigana na kusababisha majeraha na mauaji katika jamii.

Si hivyo tu Mwanamme wa Tanzania amekuwa ni mvumilivu kwa vile amekuwa
akitendewa mambo yote haya bila kuwa na chombo cha kukemea vitendo
hivi jambo lililotoa ushawishi kwa waanzilishi wa chama hiki kupata
uchungu na hatimaye kuamua kuanzisha Asasi hii.

Muda mrefu mwanaume wa Tanzania hakupata wapi pa kwenda kupata msaada
wa kisheria, imefika wakati wanaume kuwa na chama cha kuwatetea dhidi
ya unyanyasaji kutoka kwa wake zao katika nyanja mbali mbali ikiwemo
mambo ya ndoa,urithi wa mali kwa wagane, pamoja na ulezi wa watoto.

TAMRA kinaenda mbali katika kuelimisha wanaume juu ya haki zao za
msingi pamoja na kuwaelimisha juu ya wajibu wao kama baba katika
kuitunza familia yake,kuondoa mfumo dume na mfumo jike, kupiga vita
unyanyasaji kwa mke na watoto,urithi wa mali kwa wajane na wagane
pamoja na kulea watoto kabla na baada ya kufariki kwa wanandoa.
Jina la asasi: Asasi hii itajulikana kuwa ni Chama cha kutetea haki za
wanaume Tanzania/Tanzania Men's Rights Association kwa kifupi TAMRA

(1) Kuanzishwa kwa TAMRA:
Asasi ya TAMRA ilianzishwa 01/05/2012

(2) Makao Makuu.
Makao makuu ya TAMRA yatakuwa katika Mtaa wa Mpakani 'A"Kijito Nyama
Jijini Dar Es Salaam kituo cha Afrika sana Nyumba Block namba 45.

vile vile kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Jijini MWANZA

(3) Anuani ya Chama ni. Chama Cha Kutetea Haki za Wanaume Tanzania.
S.L.P 60065
Dar Es Salaam - Tanzania
Simu: Mwenyekiti TAMRA TAIFA +255 784 203 556
Katibu Mkuu TAMRA TAIFA +255 787 565 533
Baruapepe: tamratanzania@gmail.com
Blog: yetu ni www.tamratanzania.blogspot.com

TAFSIRI

"TAMRA" itamaanisha ni TANZANIA MEN'S RIGHTS ASSOCIATION.
KUTAKUWA NA VIONGOZI WAFUATAO WA TAMRA
· Kutakuwa na Mwenyekiti wa TAMRA Taifa.
· Katibu mkuu wa TAMRA Taifa.
· Mweka Hazina wa TAMRA Taifa.
· Katibu wa Uhamasishaji wa TAMRA Taifa.
· Wajumbe wa Bodi ya TAMRA

KAZI ZA TAMRA.

TAMRA itakuwa na kazi zifuafuatazo:
(1) Kutetea wanaume dhidi ya unyanyaswaji katika ndoa.
(2) Kutoa elimu juu haki za Wanamme
(3) Kuwaelimisha wanamme kuondokana na mfumo dume/jike.
(4) Kuelimisha wanaume kuhusu haki na usawa kati ya mwanamme na
mwanamke katika kutoa maamuzi kwa mambo mbalimbali ya kifamilia,
kisiasa na kiuchumi.
(5) Umiliki wa mali katika familia.
(6) Haki ya kushiriki na kufurahia ndoa.
(7) Kuelimisha jamii juu ya Haki ya kumiliki mali kwa pamoja kabla na
baada ya kifo cha mmoja wa wanandoa.
(8) Kuelimisha wanandoa kuhusu Haki na wajibu wa kuheshimiwa na
kupendwa kwa kila mwanandoa kama ilivyo katika maandiko matakatifu
bila kuathiri itikadi za dini.
(9) Kuhakikisha kwamba TAMRA inashirikiana na taasisi za kutetea haki
za wanawake ili kuondoa imani potofu dhidi ya mwanamme ili kujenga
mahusiano mazuri katika familia badala ya kuchochea uhasama kwa
kumkandamiza mwanamme kuwa ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya familia.
10.kuhakikisha kuwa kuna usawa na uhuru wa kujieleza pindi mashauri ya
ndoa yanapopelekwa katika vituo vya Polisi kwa uchunguzi na hatimaye
hatua ya kupelekwa katika vyombo vya maamuzi.
11.Kuhakikisha kuwa wapo Mawakili wa kutosha panapotokea mashauri
katika Mahakama watakaotetea Haki za Wanaume ili kuhakikisha Haki
inatendeka

MALENGO YA TAMRA.

TAMRA itakuwa na malengo kama ifuatavyo:-
(1) Kupigania Haki za mwanaume katika masuala mbalimbali ikiwamemo
kulinda na kudumisha ndoa.
(2) Kulinda Haki ya mwanaume ngazi ya familia ,kitaifa na kimataifa.
(3) Kuelimisha waathirika wa unyanyasaji
(4) Kutoa msaada wa kisheria Bure kwa kutumia mawakili wa TAMRA.
(5) Kutoa elimu ya Afya na malezi ya mtoto wa kiume ili akue katika
maadili yanayozingatia haki sawa kwa wote kuondoa dhana ya mfumo dume.
(6) Kutoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa
yasiyokuwa na tiba ikiwamo Ukimwi (HIV/AIDS).
(7) Kutoa elimu na mafunzo kwa wanamme ili kuwafundisha ujasiria mali
kuondoa utegemezi .
(8) Kufanya upatanishi na usuluhishi kwa wanandoa kwa kuzingatia
mila,Desturi,Dini pamoja na sheria za Nchi.
(9) Kutoa elimu kwa wanaume kukubali mabadiliko ya mwili kufuatana na
umri kuwa mkubwa kati ya mwanamme na mwanamke.
(10) Kulinda Haki za kila raia bila kujali itikadi za dini, rangi,
kabila jinsia na taifa.
(11) Kutoa Elimu ya uraia.
(12) Kushirikiana na serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa
katika maadhimisho ya siku ya mwanamme Duniani ikiwemo kuandaa
sherehe hizo kitaifa kufuatana na kalenda ya kimataifa kila mwaka.
12 Kutoa misaada kwa makundi ya wasiojiweza yatima,
wazee,wagonjwa ,wakimbizi majeruhi wa ajari, majanga kama njaa,
mafuriko, shule au kujenga majengo ya kutoa huduma za afya na elimu
kulinda na kutunza mazingira kuangalia chaguzi ndani na nje ya
Tanzania.


USIKOSE KUSIKILIZA KIPINDI MAALUM KATIKA RADIO NURU FM SIKU YA
JUMAMOSI TAREHE 9 KITAKACHORUSHWA KUANZIA MIDA YA SAA 3.20 -4.00 USIKU
TUTAKUWA NA MWANASHERIA WA TAMRA BW.BENY SHABAKAKI

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments