[wanabidii] FastJet : Madai yanayotukabili ya kunyang’anywa leseni hayana ukweli wowote

Friday, February 08, 2013
Pamoja na habari katika magezeti ya leo, biashara ndani ya kampuni ya
FastJet inaendelea kama kawaida na ndege zetu katika nchi ya Tanzania
kama kawaida na bado tunazidi kuzindua vituo vipya kama ilivyopangwa.

Madai yanayotukabili ya kunyang'anywa leseni ni uzushi wa baadhi ya
watu au kampuni zenye chuki dhidi ya kampuni ya FastJet, kusudi lao ni
kudhoofisha uaminifu na kuharibu sifa ya jina la biashara na bidhaa
zetu za fastjet.

Ofisi zetu na vituo vyetu vya kuuzia tiketi bado viko wazi kwa ajili
ya bookings na kwa tiketi zilizolipiwa pesa haitarudishwa.

Kwa maelezo zaidi tafadhali soma hapo chini:

7th February 2013
Fastjet plc
("fastjet" or the "Company")
Brand Licence

Kwa mujibu wa taarifa zilizo potofu kutoka kwenye vyombo vya habari,
David Lenigas, Mwenyekiti wa fastjet plc na Mwenyekiti wa Five Forty
Aviation Limited (Kenya) ("FLY540 Kenya), anathibitisha kwamba hakuna
Mikataba halali yoyote kati ya fastjet na Fly540 juu ya jina la
biashara au uongozi

Kauli yaliyotolewa na Don Smith kutoka Kenya, mkurugenzi wa Fly540
Kenya, kupendekeza kuwa ana haki ya kuondoa jina la biashara sio jambo
la kweli na lisilo na msingi wowote. Bodi ya Wakurugenzi wa Fly540
Kenya hawajawahi kulifikiria suala hili.

FastJet ingependa kuvishauri vyombo vya habari na abiria wetu ambao
wanaendelea kusafiri na ndege za fastjet na Fly540 barani Afrika,
kwamba tunatarajia kupanua huduma zetu za gharama nafuu katika Bara la
Afrika.
via FastJet.com/Tz
+255 685 680533 / +255 658 680533 / +255 767 00790


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2KJ6DJcJT

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments