kwa sasa. Habari ya kusikitisha iliyopo sasa ni ya wanafunzi wa kiume
sita wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mbuyuni, Wilaya ya
Kinondoni Dar es Salaam kubainika kuwa wana tabia ya kulawitiana.
Hili ni doa kubwa sana la kimaadili miongoni mwa wanafunzi. Kabla ya
tukio hili, matukio mengine yaliyowahi kulipotiwa siku za nyuma (ndani
ya miaka 3 iliyopita) ni ulawiti wa watoto wadogo wanaosoma madarasa
ya chini (darasa la kwanza hadi la nne) katika baadhi ya shule za
jijini-kati Dar es Salaam. Watoto hao walikuwa wakifanyiwa unyama huu
na watu wazima-ambao wendawazimu wao unawatuma 'kufurahi' wanapokuwa
wakilawiti watoto wadogo. Hivyo basi-tatizo hilo bado lipo, hata kama
halilipotiwi katika vyombo vya habari siku za hivi karibuni. Huenda
wahuni hawa wamefanikiwa kuongeza usiri wa vitendo vyao viovu.
Matukio haya ya kimaadili-ambayo pia ni kinyume cha utamaduni mwa
watanzania lazima yakomeshwe. Tufanyeje? Wazazi wana jukumu muhimu la
kufuatilia mienendo ya watoto wao na kuwaonesha njia sahihi kwao
kuifuata. Ni muhimu mzazi kuhakikisha kwamba mwanao hajengi ukaribu na
marafiki ambao wana tabia zisizoridhisha. Hata hivyo walimu (na hata
kamati za shule) wana nafasi muhimu sana wa kutengeneza mazingira
salama kwa watoto wakiwa shuleni. Hili nalo linaweza kuongezewa nguvu
na elimu ya watoto kujitambua ili waweze kuepuka vishawishi au
mazingira hatarishi.
Kwa bahati mbaya kutokana na umri wao mdogo, baadhi ya watoto
wanabakwa au wanashawishiwa kufanya vitendo hivi bila kujitambua kuwa
wanafanya au kufanyiwa kitendo hatari. Wengine huamua kukaa kimya-hata
kama hawapendi kile wanachofanyiwa. Ni muhimu pia kwa wazazi
kuwafundisha watoto wao wa kiume na kike namna ya kujihadhari na
matukio ya namna hii; na pia kuwaelimisha madhara makubwa wanayoweza
kupata. Elimu ya aina hii imekuwa haitolewi kwa utoshelevu hasa kwa
watoto wa kiume; kwa mtazamo kwamba-hawatapata matatizo. Tuamke Sasa;
Tuanze Sasa kuwapa hadhari muhimu ili kulinda usalama wao na heshima
yao.
https://www.facebook.com/hakielimu
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments