[wanabidii] Matokeo ya Kidato cha IV kwa idadi

Tuesday, February 19, 2013
Angalieni balaa hili:
 
Div I = 1,641
Div II = 6,453
Div III = 15,426
Div IV = 103,327
Div 0 = 240,903
 
Si kweli kwamba kupata Div IV ni kufaulu; ni upumbavu tu kusema kwamba mtoto amefaulu kwa Div IV kwa sababu hana pa kwenda labda ualimu wa shule ya msingi kama bado wanawachukua. Kimsingi waliofeli ni Div IV na Div 0 ambao ni jumla ya 344,230 kati ya 367,750, yaani asilimia 93.6 wamekwama.
 
Div ni 0.45% ya wanafunzi wote. Hawa ndiyo watoto waliofanya vema kama tunataka kuwa wakweli.
 
Maskini Tanzania yetu; tutajenga taifa gani na vilaza hawa mamia ya maelfu???
 
Matinyi.

Share this :

Related Posts

0 Comments