Chadema yalaani mauaji ya kidini, kuzindua sera ya majimbo leo
18th February 2013
B-pepe
Chapa
"Udini ni sera ya CCM, wamelikoroga, sasa tunataka walinywe," alisema jana wakati akifungua mkutano wa viongozi wa majimbo 33 na mikoa ya Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, ikiwa ni sera yao ya majimbo.
Pamoja na kuwaonya viongozi, Mbowe pia aliwataka wanachama wa Chadema popote pale walipo wasishiriki kuwabagua wenzao kwa imani ya dini bali waheshimu imani za watu wengine.
Aidha Mbowe alisema; "Chadema inalaani vikali mauaji ya viongizi wa dini yanayotokea maeneo mbalimbali nchini…tunaitaka CCM na serikali yake kuwajibika dhidi ya mauaji hayo."
"Kuona kiongozi wa dini akimwagiwa tindikali, akipigwa na hata kuuawa kwa sababu za kidini sio mambo ya kujivunia hata kidogo…CCM ndiyo iliyokuwa ikilea udini na hapo ndipo ilipotufikisha…tunataka CCM na serikali yake iwajibike kwa hilo."
Alisema Mkristu hana haki ya kumhukumu Mwislamu na wala Mwislamu hana haki ya kumhukumu Mkristu, hivyo Chadema kimeamua kuchukua hatua kali dhidi ya mwanachama ye yote bila kujali wadhifa wake atakayehamasisha chuki za kidini.
Alisema sera ya udini iliaasisiwa na CCM kama mbinu yao ya kuwafanya waendelee kubakia madarakani lakini hali inavyoonekana sasa inatisha amani na umoja wa taifa.
0 Comments