Ndugu zangu,
Tangu tume"shauriwa" kuruhusu uchumi huria na kuachia ushindani, yaani biashara iwe ya ushindani(japo sisi hatukuwa na cha kushindanisha), ndipo viwanda vyetu vikabidi kufa.
Kufa kwa viwanda kukapukutisha ajira kwa watanzania walio wengi. Kukosekana kwa ajira kukaenda sambamba na kupanda kwa gharama zote kutokana na serikali "kushauriwa" tena kuondoa ruzuku, nk.
Tangu "tushauriwe" hivyo, kila uchao tunasifiwa kuwa uchumi unakua. Ukuaji wa uchumi wetu umejikita kwenye uzalishaji gani endelevu? Madini na miradi mingi ya wawekezaji inategemea rasilimali zinazoisha(diminishing resources). Dhahabu na almasi vikiisha, tutakwenda wapi, na haya madeni tunayolimbikiza kila siku, yatalipwa na nini?
Mbona nchi zilizoendelea, hujulikana pia kama nchi zenye viwanda? Vya kwetu viko wapi, na tunaedeleaje kama taarifa zetu zote za kukua kwa uchumi hazizungumzii non-perishable activities kama hizo za viwanda? HIvi hakuna shida hapa? Wachumi watusaidie
Naomba kuwasilisha wajameni!
MJL
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments