[wanabidii] Dr Slaa anaweza Kuitosa Chadema isipomteuwa 2015

Saturday, January 19, 2013
Ndugu zangu

Dr Slaa aliwahi kuwa padre lakini baadaye akalitosa kanisa akaamua
kutumikia dunia kwa kujipatia jiko na maisha mengine ya kidunia .

Amewahi kumtosa Mke wake wa kwanza ambaye wamewahi kufikishana
mahakamani kwa ajili ya kupinga ndoa yake mpya na kuomba matunzo ya
watoto aliowatosa .

Miaka ya 90 Dr Slaa Aliitosa CCM Baada ya kushindwa kwenye kura wakati
alipotaka kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la karatu .

Sasa tunaelekea mwaka 2015 ambapo tutakuwa na uchaguzi mkuu wa wabunge
na rais nchini na inasemekana Dr Slaa anaweza akakosa nafasi hiyo ya
kuwakilisha chama katika uchaguzi wa mwaka 2015

Swali ninalouliza wadau je Dr Slaa ataitosa CHADEMA kama alivyoitosa
CCM miaka ya 90 ?

Swali hili limenijia maana amewahi kufanya maamuzi mazito 3 na
kuendelea na maisha tu .

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Related Posts

0 Comments