[wanabidii] Ushindi wa Dialo, Je ni ushindi wa Mtandao mpya

Wednesday, October 17, 2012

Habari wanajukwaa, jana uchaguzi wa CCM Mwanza ulifanyika na mkiti mpya ni Antony Diallo, aliwahi kuwa Mbunge wa Ilemela.
Ushindi wake umezua maswali mengi kama ataweza kuwaunganisha wana CCM ukizingatia huko nyuma akiwa mbunge alikuwa na tuhuma nyingi 
moja wapo ni kuwagawa wabunge wa mkoa wa Mwanza hasa pale walipotaka kuwa na sauti moja kuleta umoja na kutetea ajenda yenye maslahi kwa Mwanza.

Diallo atakuwa "kaziliwa mara ya pili" ili alete umoja au ndiyo mwendelezo wa siasa za ubabe na jeuri ya fedha iliyompa ushindi?

Kumbuka mtandao uliomwingiza JK madarakani baadhi ya wadau wake leo hii pia wamo katika harakati kama za wakati ule kuingiza safu za wagombea watakaoshinda kwa malengo ya kupata uteuzi wa Urais 2015.

Kilichotokea Mara ni kama Mwanza. Makongoro alianguka kwa shinikizo la "wakubwa" waliomwaga fedha kwa wajumbe wa mkutani mkuu vilivyo,
hali kadhalika juzi na jana kati ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Mwanza fedha wamepewa mpaka unajiuliza, Uenyekiti una maslahi gani kifedha ili
"utapowekeza" upate faida katika mtaji wako 

Share this :

Related Posts

0 Comments