miaka 35
sasa.
Nilijiunga na Chadema kwa matumaini niliyokuwa nayo kuwa ni chama
kitakachomkomboa Mtanzania kutoka kwenye umasikini na kumfikisha
kwenye
level sawa na watu wa mataifa mengine kama Botswana , Namibia au hata
baadhi ya nchi za Ulaya.
Niliamua haya baada ya kufuatilia yanayoandikwa kwenye vyombo vya
habari
kwa sababu mie binafsi kwa sasa naishi UK hivyo basi mambo mengi
yatokeayo
nyumbani huwa nayapata kwa kusoma magazeti na blogs mbali mbali.
Nilifanikiwa kukutana na Mheshimiwa Lema hapa London ambapo tukapanga
mikakati ya kukijenga chama hapa UK na nikapewa jukumu la kufungua
matawi
nchi nzima na kuhamasisha Watanzania, kazi ambayo niliifanya kwa moyo
mmoja. Pia nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chadema UK.
Nimefanikiwa kuhamasisha watu wengi na baada ya miezi michache
niliamua
kwenda nyumbani kuona hali ilivyo. Niliyoyakuta ilikuwa tofauti na
niliyokuwa nikiyasikia na kusoma.
NIMEKUTA BARABARA NZURI SIJAWAHI KUONA TOKA NIZALIWE NA ZINAENDELA
KUJENGWA!
SHULE ZA SEKONDARI KILA KATA NA VYUO VIKUU VYA KUJICHAGULIA.
MAISHA YA WATANZANIA YAMEBADILIKA SANA - MIDDLE CLASS NI MAISHA YA
KAWAIDA
TU. VIJANA WENGI WAMEENDELEA TOFAUTI NA ZAMANI MPAKA UWE MCHAWI KIDOGO
NDIO
UWE TAJIRI. MIJI INAJENGEKA KWA KASI YA AJABU. UKIHARIBU KAZINI
UTAWAJIBIKA
.
Na mengine mengi tu niliyaona mpaka nikaanza kujiuliza , hivi najiita
mpinzani, NINAPINGA NINI?
Kama ni maendeleo nayaona tena maendelo original Nikakumbuka msemo
mmoja...
"KWA NINI UHANGAIKE NA FOTOKOPI WAKATI ORIGINAL IPOO?"
Kwangu mimi CCM ni original na Chadema ni photocopy, tena copy
iliyotolewa
wakati mashine imekwisha wino . Mabadiliko ya kweli yatatokea ndani ya
CCM
na si kwingineko!
Kuna mengi mazito yamenichefua Chadema lakini sitayasema leo. Juzi
mwenyekiti wangu wa Taifa Mheshimiwa Mbowe alipita hapa UK, lakini,
mpaka
ameondoka hakutaka kuwasiliana na kiongozi yoyote wa Chadema hapa UK
kitendo ambacho kiliniuma sana, kwani, niliona kama tumedharauliwa;
BABA HUWEZI KWENDA SEHEMU WALIPO WANAO UKASHINDWA HATA KUWAPIGIA SIMU
KUWAJULIA HALI.
Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wangu utaeleweka. Kama tujuavyo, kila
kwenye
msafara wa mamba na kenge wamo, lakini naona kwenye msafara wa
Chadema
idadi ya kenge inazidi mamba.
Chris Lukosi
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments