[wanabidii] Yanga yatoa taarifa ya mapato na matumizi

Wednesday, November 14, 2012

Timu ya Yanga ya Dar es Salaam ambayo inaongoza ligi ya Kabubu
nchini Tanzania leo hii imetoa takwimu zake za mapato na matumizi
katika vyombo vya habari na kuonyesha kile kilichopatikana na
kutumika kwa miezi ya Julai hadi Oktoba mwaka huu.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kwa kipindi hicho timu ya Yanga
ilipata Shilingi Bilioni 1.042 kutoka vyanzo mbalimbali, ikiwamo
pesa zinazotokana na viingilio, udhamini,zawadi za ushindi, malipo
ya uanachama kwa kilabu hiyo kongwe nchini na vyanzo vingine.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa bado Kilabu hiyo kongwe inategemea
ufadhili ambapo kwa muda huo zaidi ya milioni mia sita
zilipatikana kwa ufadhili pekee ambayo ni sawa na nusu na ushehe
wa fedha zote zilizokusanywa.

Kilio bado kipo kwani shilingi milioni 2.53 zilipatikana kwa malipo
ya kadi za uanachama ambapo ni kiwango cha chini mno cha fedha
zilizopatikana kwa vyazo vyote..

Matumizi yake yananaonekana kuwa gharama kubwa zipo katika
usafirishaji wa timu ambapo kwa kipindi hicho zaidi ya shilingi
milioni 598 zimetumika.

Japokuwa mimi ni mpenzi wa Simba nimevutiwa mno na utaratibu huo wa
Yanga wa kutoa mapato na matumizi yake kwa kipindi hicho.
Nawapa pongezi Ynaga kwa hilo, hongereni wana Jangwani, basi
jukumu la kila timu na kila sekta ambayo inahusisha mali ya
jamii au vikundi kuweka wazi mapato na matumizi kwa lugha nyepesi
ili jamii kujua utendaji wa kikundi hicho.


Wasalaam Adeladius Makwega.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Related Posts

0 Comments