[wanabidii] "Profesa Wangu Kitila Mkumbo Hapa Sijakuelewa Vema..!"

Friday, January 16, 2015

Mdahalo kwa wanaotajwa urais una maana gani?
Nina maswali mengine;
- Je, hatuoni kuwa kwa wanaojitaja urais au kutangaza nia wanapoandaliwa mdahalo ni sawa na kujifanyia kampeni za wazi kabla ya kipenga kupulizwa?
- Je, kama wanaojitaja au kutangaza nia si wagombea binafsi, bali wa vyama, hatuoni kuwa ni ajabu kuwa watashiriki mdahalo bila ya ilani za uchaguzi za vyama? Ina maana wata-debate juu ya namna watakavyotekeleza ' ilani za kusadikika'?!
Maswali ninayo mengi kwa Profesa Mkumbo ambaye ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanataaluma, Udasa. Waandaaji wa mdahalo.
Hili la mdahalo ni jambo jema kabisa, wasiwasi wangu tusije tukapoteza maana ya mdahalo. Kwamba kusanyiko la watangaza nia laweza kuwa ni usaili wa wazi tu wa watangaza nia badala ya kuita mdahalo. Na kama lengo ni kuwafanya watangaza nia wafahamike na wapiga kura, tukubali , kuwa kama mtangaza nia ya kugombea urais, ikiwa imebaki miezi tisa kupiga kura hafahamiki kwa watanzania, basi, huyo hatufai kuwa Rais Wetu...
Maggid,
Dar es Salaam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments