Subject: [UDADISI: Rethinking in Action] Tupigie Kura (Referendum) Lugha ya Kufundishia?
UFUATAO NI UCHAMBUZI MFUPI WA MFUATILIAJI WA KARIBU WA UKUSANYAJI WA MAONI YA WANANCHI WA TANZANIA KUHUSU KATIBA MPYASuala la lugha ya kufundishia linaibuliwa sana katika maoni. Kwa usikivu wangu ninahisi watu wengi wanapendelea Kiswahili kitumike hata vyuoni. Lakini wako wanaopendelea Kiingereza.Kinachodhihirika kwangu ni mgawanyiko ulioko unaotokana zaidi na matabaka. Wale wanaotumai kuwa watoto wao watafanya kazi majuu au kwa vibaraka wa nje wanatetea sana hoja ya Kiingereza. Wale wanaohitaji kuwa huduma ziwafikie kwa lugha nyepesi na wapate ufahamu wa nini kinaendelea katika maisha yao wanapendelea zaidi Kiswahili kitumike. Na kuna wale bado ulimbukeni umewasakama kwa kuona ustaarabu ni kunena Kiingereza au kurashia maneno mawili matatu ili nao waonekane wamo.Suala linalozungumzwa sambamba na hili ambalo linatofautiana ni lile la lugha ya taifa. Hapa ndipo hoja za kukitukuza Kiswahili au kudumisha utaifa zinapoangushwa. Suala la lugha mama halinogi vyema (si vema jamani) kwa baadhi ya wazalendo ambao wana lugha zao mama ambazo si Kiswahili na kamwe hatusemi Kiswahili kitawale lugha nyingine na kwa namna hii basi kama vile tunavyodhani Wakenya au Waganda wanaunganishwa na lugha ya kigeni, yaani Kiingereza, basi sisi tujivunie kuwa kuna lugha ya Kiafrika inayotuwepesishia mawasiliano.-- Posted By Blogger to UDADISI: Rethinking in Action at 11/24/2012 02:36:00 AM
Related Posts
- [wanabidii] AJALI YA BODABODA YAUA WAWILI MKOANI GEITA
- [wanabidii] East Africa: AfDB rolls out the first capacity building program on Value for Money in Social Service Delivery in East Africa
- [Mabadiliko] Internship (f/m) – Life Cycle Assessment / Sustainability Assessment / Environmental Impact / Ecological Impact / Input-Output Analysis
- [wanabidii] African Business Magazine releases its survey of Africa's most valuable brands
- [Mabadiliko] Master Student (f/m) – Life Cycle Assessment / Sustainability Assessment / Environmental Impact / Ecological Impact / Input-Output Analysis
- [wanabidii] LIPUMBA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA DENMARK NA KUJADILI UCHUMI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments