[wanabidii] TAARIFA KWA UMMA JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI NCHINI TAREHE 18.09.2012

Wednesday, September 19, 2012
KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA:

TAARIFA KWA UMMA JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI NCHINI
TAREHE 18.09.2012

Kamati ya Jumuiya ya Madaktari Nchini , kwanza inapenda kutoa pole kwa
Wanahabari wote nchini kwa kitendo cha kinyama ambacho Mwanaharakati
na Mwandishi wa habari, Marehemu David Mwangosi alifanyiwa, hii ni
ishara kuwa Jeshi la Polisi wameamua kutumia njia ya kuua raia ili
kujenga hofu na woga miongoni mwa wapenda demokrasia na maendeleo
nchini.

Pia tunapenda kulaani kitendo cha Serikali kupitia Wizara ya Michezo,
Habari na Utamaduni kulifungia gezeti makini la Mwanahalisi kwa sababu
ya kutoa taarifa za ukweli juu ya waliotaka kukatiza uhai wa
Dr.Ulimboka Stephen, Jamii ya Madaktari na watanzania wengi bado
wanaamini kuwa waliotajwa na gazeti la Mwanahalisi ni miongoni mwa
waliohusika na kutekwa, kuteswa na kutelekezwa kwake na si yule
anayesemekana kuwa na matatizo ya akili aliyedaiwa kukamatwa na
Suleimani Kova. Hivyo tunalitaka Jeshi la Polisi litoe ripoti yake ya
Uchunguzi ili kubaini ukweli wa taarifa hii.

Pia, tunachukua nafasi hii kupongeza mshikamano ambao Madaktari
wameendelea kuuonyesha licha ya changamoto nyingi tunazopitia, ni vema
ikafaamika kuwa ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa MAT na
MAT imefunguliwa kesi 2 mahakamani, Ni katika kipindi hiki ambacho
zaidi ya interns 300 wanasubiri kuitwa kuhojiwa na MCT bila kujua ni
lini hilo litafanyika, Ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Madaktari anapata mapumziko baada ya kutoka katika Matibabu
nchini Afrika Kusini, lakini ni katika kipindi hiki ambacho mpaka sasa
hakuna hata hoja moja ya Madaktari imefanyiwa kazi na Serikali.

Tunapenda ieleweke kuwa suala la madai ya Madaktari si tukio, ni
mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ndio maana
tumeshuhudia migomo hii katika nyakati tofauti pamoja na kujitokeza
kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha
taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini
na maslai ya watumishi kwa ujumla.

Kuhusu suala la interns, Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 10, Julai 2012,
Baraza la Madaktari Nchini lilitoa taarifa kwa umma kuwa imesitisha
leseni za muda kwa Madaktari waliochini ya mafunzo kwa vitendo, pia
waliahidi kuwaita kwa nia ya kuwahoji mmoja mmoja pindi
wakatapokamilisha uchunguzi wao, cha kushangaza ni kwamba miezi 2 sasa
imepita bila hilo kufanyika.

Katika vikao mbalimbali ambavyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Naibu wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, na Kaimu Katibu Mkuu
wameshiriki, wamekuwa wakisisitiza kuwa hili lipo kisheria na interns
wasuburi kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa. Hivyo tunapenda kutumia nafasi
hii kuitaka MCT itekeleze kwa haraka majukumu yake kwa lengo la
kuharakisha upatikanaji wa haki.

Hivyo basi Kamati ya Jumuiya ya Madaktari imejiandaa vya kutosha na
taratibu za kisheria na itahakikisha inaweka wakili pale interns
watakapoanza kuhojiwa kwa kuwa sheria inayounda MCT inatoa hiyo
nafasi.

Mwisho kabisa tunapenda kutoa wito kwa interns kutumia hekima na
busara katika kipindi hiki kigumu, waepuke kutumiwa na kikundi cha
watu ambao wanatumika au wanajitumia kwa maslai ya kustarehesha
watawala.

IMETOLEWA NA;
KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Related Posts

0 Comments