[wanabidii] Rais Jakaya Kikwete Amteua Rished Bade kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA

Wednesday, September 19, 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Bwana Rished Bade kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Septemba 19, 2012 na Ofisi ya
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais - Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza Jumatatu
wiki hii, Septemba 17, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Bade alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Tanzania Mortgage Finance Co. Ltd.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Septemba, 2012

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

Share this :

Related Posts

0 Comments