[Mabadiliko] PALE CCM INAPOFUNIKA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI!

Monday, May 01, 2017
Leo nimemshangaa sana Rais Magufuli alipokuwa akifurahia mahudhurio ya "wafanyakazi" kwenye sherehe za Mei Mosi wakati mle uwanjani walikuwa wamejaa makada wa CCM na alikuwa akiwaona mubashara bila chenga kwa kuwa walikuwa wamevaa sare za CCM. Ni taahira pekee anayeweza kuamini kwamba yale makofi na vifijo vilitoka kwa wafanyakazi.
.
Kinachoudhi mno katika maadhimisho haya ya kitaifa ni kuyaona maCCM yamevaa sare na yamejaza uwanja utadhani ni mafanyakazi. Ifike wakati haya majitu yatambue mipaka yao. Rais Magufuli amehudhuria pale kama Rais wa JMT, sio kama mwenyekiti wa CCM. Sasa nyie magamba wa CCM mlioenda kurundikana pale uwanjani mmetunisha matumbo kama vyura ni nani aliwaita? Nyie ni wafanyakazi? Acheni hizo.
.
Na Rais alipoapa kutopandisha mishahara kwa kipindi chake chote atakachokuwa madarakani mlishangilia sana kana kwamba wafanyakazi hawastahili kupata maslahi bora kwa kazi wanayoifanya! Hivi nyie wanahizaya ni nani aliyewaroga?
.
Nashauri kunapokuwa na mkusanyiko kama huu ambao hauhusishi vyama, magamba yote yaliyovaa magwanda ya kijani na njano yazuiliwe kuingia. Haya majitu ndio yanayovuruga mambo. Rais hata kama akiongea maneno kandamizi kwa wafanyakazi, yenyewe yanamshangilia. Shame upon you!
.
Ni bahati mbaya kwamba TUCTA bado haijapata kiongozi anayejitambua. Baada ya kuondoka Mgaya, ambaye ni kada wa CCM kindakindaki, amekuja huyo mrithi wake ambaye naye anaonekana kuwa na chembechembe za CCM kwa 100%. Haiwezekani mkusanyiko wa wafanyakazi ujae makada wa CCM bila kiongozi wa TUCTA kukemea pepo hilo. Hapa iko namna. Leo nimeamini kwamba bado TUCTA haijapata kiongozi makini anayetetea maslahi ya wafanyakazi. Eti badala ya kutetea maslahi ya wafanyakazi, yeye anaenda kukazia tamthlia ya V-WONDER. Vinakuhusu? Inauma sana.

Share this :

Related Posts

0 Comments