Njia nyingine na muhimu ya lazima kwa vyombo hivi kuheshimiwa, ni vyombo vyenyewe kujiheshimu na kuheshimu nafasi zao.
Matukio mawili hivi karibuni yaliyotendwa na askari polisi wetu ni mfano mmojawapo wa jeshi hili kutojiheshimu na kwa kweli lisitegemee kuheshimiwa hata rais angeagiza.
Mkoani Pwani Polisi wamevamia kijiji cha wafugaji na kuanza kuswaga ng'ombe na kuwapeleka Polisi. Wafugaji bila kubisha wakakubali ng'ombe wapelekwe. Lakini wakataka ng'ombe hao wahesabiwe ili ijulikane ni ng'ombe wangapi wanachukuliwa. Polisi hawataki. Wanaamua kurusha risasi na kuua. Anakuja Mkuu wa Wilaya na kukana kuwa askari hao walikuwa hawakutumwa katika eneo husika maana sio eneo lenye mgogoro. Ni eneo la wafugaji. Wananchi wanadai hatua zichukuliwe kwa askari hao. Hakuna hatua zinazochukuliwa Mkoa mzima, mpaka waziri wa mambo ya ndani alipofika ndipo akaagiza askari hao wakamatwe.
Hebu tuone viashiria hivi; na kama ndio mfumo tuone kama raia wa Tanzania wako salama kweli:
1. Askari anakwenda eneo lisilo na mgogoro na bila kuagizwa na wakubwa wake wa kazi, anakamata mali za raia.
2. Raia wanakubali lakini wanataka kuhakiki mali inayokamatwa. Askari wanakataa. Wanaamua kuua raia hao.
3. Mkuu wa Wilaya anadhibitisha Polisi hao wamefanya kitendo cha kihalifu; (kwa sababu hawakutumwa huko kukamata mali za raia hao).
4. Mkoa mzima ambao una Mkuu wa wilaya, OCD, RPC na Mkuu wa Mkoa hakuna anayeona na kutumia madaraka yake kuwakamata askari hao. Maana yake wako huru na wanaweza kufanya hivyo hata kijiji kingine.
5. Amri ya kuwakamata Polisi hao inakuja kutolewa na waziri.
Hivi katika mazingira haya raia wajione wako salama??? Tanzania ina mokoa karibu 30. Mikoa kumi ikipata tatizo linalohitaji askari akamatwe mpaka waziri aisungukie yote? Nataka Mwigulu ajijibu (asitangaze jibu). Sisi tunataka kupata jibu kwa jambo atakalolitenda.
Mwigulu kuagiza askari walioua wakamatwe, amemdhalilisha RPC. Kumsheshimu RPC wake alipashwa kumtimua kazi. Nitatoa mfano. Kuna tajiri mmoja alijenga kituo cha mafuta barabarani Mwanza. Waziri Magufuli (alikuwa hajawa rais), akamwagiza Mkuu wa mkoa kukibomoa kituo hicho. Mkuu wa mkoa akakataa. Magufuli (Inasemekana) alimpigia simu na kumwambia Mkuu wa Mkoa asikilize taarifa ya habari ya saa kumi atatajwa mkuu wa Mkoa mpya atakayefanya kazi hiyo. Simu ilipokatwa Mkuu wa Mkoa (inasemekana) alikwenda kusimamia kituo kuvunjwa na kwa masaa kilikuwa hakipo tena. Tunataka tuone kinachotokea ambacho inasemekana Mwigulu alifanya (kwa RPC) wake; kama Magufuli alivyofanya kwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati huo.
Kituko cha pili ni cha wanafunzi wa Simiyu. Wanafunzi wanasema shule yao ilikuwa inashindwa. Ameletwa mwalimu kwa juhudi zake sasa matokeo ya mitihani yanaonyesha mabadiliko. Mwalimu huyo anahamishwa. Wanafunzi wakaamua kuandamana. Wamebeba makaratasi. Polisi wakaja kuwazuia wasiandamane. Ni haki kabisa kuwazuia. Ilitarajiwa Polisi waweke ukanda na kuwatangazia wasimame hapohapo na kuwahoji wanataka nini. Sasa wanakuja na zana kana kwamba watu wanauana na namna ya kuwatawanya ni kuwavurunda.
Zimetoka picha mtandaoni zikionyesha Polisi "wanamdhibiti" mwanafunzi. Huyu anavuta huku, huyu anavuta huko, huyu anapiga ngwara. Mtu unajiuliza Polisi walikuwa wanafanya nini hasa? Nani alikuwa anawaongoza wenzake kufanya hivyo? Huyu mwanafunzi angeambiwa "panda gari hilo" angepanda. Angebisha Polisi wawili walitosha kumshika na kumlaza chini na kumuweka Pingu. Ukiiangalia picha hiyo hukosi kujiuliza kiwango cha elimu kinachotolewa kwa Polisi wetu huko chuoni! Kuna mtu aliwahi kusema huwa wanafundishwa ukakamavu na gwaride tu. Ukilinganisha picha hizo na usemi huo huwezi kumkatalia aliyesema wanajifunza gwaride na ukakamavu tu. Hakuna busara ya kuwashugulikia wahalifu inatolewa. Hakuna aina ya maandamano na namna ya kuyadhibiti. Hakuna elimu ya mahusiano na raia wema ili kazi yao iwe nyepesi. Kuna mtu anauza viroba jirani yangu. Mpaka sasa najiuliza nimwambie nani? Vituko hivi ndani ya makala yangu sithubutu kumwambia Polisi. Nakubaliana na mengine yanayosemwa juu yao. Mambo haya hayawezi kuacha kutonesha vidonda myoyoni mwetu juu ya matendo ya Polisi. Mauaji ya Mwangosi; Kuburuzwa ndani Lipumba wakati amewambia Polisi kuwa anakwenda kuwatawanya watu waliokuwa hawajui kuwa mkutano umekataliwa; na mengine mengi tu.
Ninakumbuka kusikia radio ujerumani wakielezea elimu ya Polisi wao. Wanasema Polisi akikutana na mtu amelala barabarani cha kwanza wanadhani ana kisukari, au kifafa au magonjwa mengine, kabla ya kufikiri ni mlevi. Polisi wana vifaa vya kupima kuhakikisha ana shida gani. Wa kwetu watapiga mateke na kusema ni mlevi. Mwigulu. Kati ya mambo ya kutopuuza ni elimu inayotolewa kwa asiakri wetu. Madaraka na wajibu wa Polisi wetu. Lakini niseme; Nitashangaa kama RPC wa Pwani ataendelea na kazi.
Elisa Muhingo
0767 187 507
elisamuhingo@yahoo.com
--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@ googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting to this Forum bears
the sole
responsibility
for any legal
consequences of his or
her postings,
and
hence
statements and facts must be
presented
responsibly.
Your
continued membership signifies that
you agree to
this
disclaimer and pledge to abide by
our
Rules and
Guidelines.
---
You received this
message because you
are subscribed
to
the
Google Groups "Wanabidii"
group.
To unsubscribe from this group and
stop receiving
emails
from
it, send an email to wanabidii+...@
googlegroups.com.
For more
options, visit
https://groups.google.com/d/
optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone
posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences
of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented
responsibly. Your
continued membership
signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are
subscribed
to
the
Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
from it, send an email
to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options,
visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings,
and
hence
statements and facts must be presented responsibly.
Your
continued membership signifies that you agree to
this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed
to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments