[wanabidii] VITA YA MADWA YA KULEVYA: WABUNGE WETU WAKO UPANDE GANI?

Tuesday, February 14, 2017
Vita ya madawa ya kulevya imeanza rasmi. Si kuwa hakukuwa na juhudi huko nyuma. La. Ila sasa imeanza na msukumo mpya. Imeanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paulo Makonda kuwataja watu wanaohisiwa kujihusisha na madawa hayo. Mwanzoni alibezwa na kuambiwa anacheza na dagaa. Baadaye akaongeza kwa kutaja majina makubwa zaidi. Hapo ndipo hasa misimamo tofauti ilionekana. Wengine wakasema hawawezi kwenda kwa sababu Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kushughulikia madawa ya kulevya. Wapo waliotaja hasara watakayoipata kwa kuitikia wito wa Makonda na vitisho vingine vingi.
Madawa haya yameharibu vijana na yanaendelea kuwaharibu. Vijana wasomi, wasanii wakishajiingiza katika madawa basi wanaharibika na kupoteza mwelekeo. Namfahamu kijana aliyekufa baada ya kunywa dawa za kilimo zilizokuwa zimetunzwa na wazazi wake nyumbani. Huyo kijana alikuwa anamalizia degree yake ya kwanza ya computer engineering. Alifukuzwa mara mbili kwa sababu ya kuharibikiwa akili baada ya kutumia madawa ya kulevya. Alipokosa madawa na bangi ikawa haimtoshi akaanza kunywa dawa hiyo kidogo kidogo mpaka ilipomuua; na wazazi waligundua baadaye sana. Madhara mengi tu huenda kila mmoja ana mifano yake. Jingine lililo wasi ni habari kuwa wahusika wakuu wa biashara hii ni wanasiasa; Wafayabiashara wakubwa na wasanii. Katika orodha ya Makonda makundi hayo yote yalitajwa.

Kati ya maneno aliyokaririwa akitumia Ndugu Makonda ni kusema Wabunge (Nadhani baadhi) ni wapuuzi na kuwa hufanya kazi ya kulala bungeni.
Wakati ukweli ukiwa kama nilivyoutia katika utangulizi, Wabunge na Bunge lilitoa msimamo kuhusu maneno ya Makonda. Maneno yoyote aliyotamka mtu au taasisi yanawakilisha msimamo wake kuhusiana na vita ya madawa ya kulevya. Wabunge wetu walijibu juhudi za Makonda kwa kuzingatia zaidi maneno yake kuhusu wabunge badala ya lengo lake la kupiga vita madawa ya kulevya. Sipendi kuungana na Makonda kuliudhi bunge letu lakini nataka kujielekeza kuhusu matukio yanayoweza kutumika kulishtua bunge (likitaka kushtuka) na kubadili mwelekeo.
Mifano:
1 Bunge limetunga sheria kadhaa kuharamisha madawa ya kulevya ikiwemo bangi. Siku moja mbunge mmoja alisimama bungeni na kusema kwao bangi ni halali hivyo ihalalishwe. Je huu si upuuzi kwa mbunge kutamka hivyo? Kama ni upuuzi; yeye aweza kuepuka kuwa mpuuzi? Lakini Baada ya neno kama hili kutamkwa na mbunge, wabunge wengine walipitisha azimio gani kuhusu upuuzi huo? Reaction ya bunge zima kuhusu neno la mwenzao ndilo linarejesha heshima ya bunge au kuiondoa.

2 Lakini tumtafakari mwakilishi mwingine. Kama mbunge kuitwa mpuuzi ni kosa na utovu wa heshima na madaraka ya Bunge, bila shaka viongozi wa miimili mingine pia. Sasa mtu anasimama na kusema Rais ni Dictator uchwara. Mtu huyo anasimama na kusema Tanzania inaongozwa na rais wa ajabu ajabu. Kosa la rais ni kusema taifa halijafikia mahala pa kuomba chakula kwani japo kuna ukame lakini mvua zinazoendelea zaweza kutumika kulima chakula kinachopungua! Maneno kama hayo japo yametamkwa nje ya Bunge lakini kwa sababu yametamkwa na Mbunge ningetarajia bunge kuwa na tamko. Kama Bunge likimrudi mwenzao kama tulivyoona huko nyuma linaweka msingi wa kutoitwa bunge la wapuuzi.

3 Nchi yetu ilipata uhuru 1961. Kabla ya uhuru nchi hii imepitia historia ya ajabu. Zamani za kale nchi ilikuwa ni chiefdoms ndogo ndogo. Watu fulani wakakaa na kuziunganisha hizo kabila na chiefdoms na kutengeneza kitu kinaitwa Tanganyika. Baada ya uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, viongozi tuliowachagua wakafanya uamuzi wa kuziunganisha nchi mbili zilizokuwa huru. Sasa ni taifa moja. Linaitwa Tanzania. Tumelitengeneza wenyewe. Lina katiba yake. Linatambuliwa hivyo. Lina changamoto zake ndiyo maana tunajadiliaana namna bora ya kuliimarisha na kuliendeleza. Ni mfano bora wa kujivunia. Africa inajivunia. Ni matokeo ya kazi tuliofanya sisi bada ya uhuru. Tanzania si ya kwanza kuungana duniani. Mfano mmojawapo ni Marekani. Iliunganisha mataifa zaidi ya 50. Kuliwahi kutokea wapuuzi fulani wakati wa utawala wa Abraham Linchoin wakitaka kulitenga taifa (jimbo) lao. Walipata kichapo kikali hawajathubutu tena. Naamini hakuna Mmarekani anaweza kuhoji muungano huo akaishi. Sisi tuna binadamu mmoja. Tena ni mbunge wa bunge letu linalostahili kuheshimiwa. Akasema Zanzibar inatawaliwa na Tanganyika. Na upuuzi mwingine mwingi tu. Mbunge huyo aliapa kiapo kuulinda Muungano. Sasa je kitendo chake hicho si cha kipuuzi? Kama ni cha kipuuzi, yeye sio mpuuzi? Bunge limetoa msimamo gani kuhusu matamshi ya mwenzao? Je Bunge kumnyamazia mbunge wa namna hiyo sio kitendo cha kipuuzi? Nakumbuka Speaker aliyepita aliwahi kuwafyatukia wananchi kuwa bunge linastahili kuheshimiwa baada ya wananchi kuwashambulia wabunge kutoana na matamshi ya ajabu. Alitumia kifungu hikihiki kinachombana Makonda. Alizimwa na wananchi walipomvamia kwenye vyombo vya habari. Alichofanya ilikuwa kuwabana wabunge wajiheshimu ili taswira yao mbele ya umma wanaowakilishwa bungeni isiendelee kudhalilika.

4 Nchi yetu; kama zilivyo nchi nyingine duniani, inakabiliwa na janga la madawa ya kulevya. Vijana wetu wameharibika na kwa kweli huo ni uharibifu wa nguvukazi ya taifa. Inatarajiwa kuwa wananchi, viongozi wataungana kupiga vita uharibifu huu. Sababu zi wazi kwa nini watu wote kuungana. Licha ya uharibifu uliopo lakini wanufaika wana uwezo mkubwa kumnunua yeyote. Katika vita kama hii lazima usemi wa Bush baada ya shambulizi la Septemba 11 litumike: "Kama hauko nasi uko kinyume nasi". Vita hii ngumu. Kuna waliojaribu na kuishia kusema wanayo orodha ya wahusika. Hawakutaja hata jina moja. Sasa amejitokeza kijana mdogo. Akawa jasiri kuwataja watu wanaojihusisha na biashara hii. Kukanyagana ni jambo la kawaida katika msafara wowote. Mtu kuamua kuingilia safari kwa sababu ya kukanyagwa haiingii akilini. Kitendo cha wabunge wetu kuungana kutaka mtu aliyethubutu aondolewe kazini, si cha kawaida. Wabunge kusema wizara husika zipo na Mkuu wa mkoa haimhusu, ni ishara mbaya. Haiingii akilini kuwa viongozi wetu wanaweza kuonekana wanadhoofisha juhudi za serikali kushughulikia janga hili.

Kimsingi kila mtu anastahili heshima. Kuheshimiwa kukubwa huanza kwa mtu kujiheshimu. Taasisi pia. Kama bunge haliwezi kufanya upuuzi hakuna anayeweza kulidhania hivyo. Kama wakifanya upuuzi, hata kama hakuna aliyewaita haimaanishi kuwa sio. Kwa kuzingatia kuwa wabunge ni wanansiasa, na ilitarajiwa wabunge kama wanasiasa kuwa waangalifu katiko hoja zao. La sivyo licha ya kuitwa wapuuzi kwa haki, haiwezekani wapiga kura wasitake wawakilishi wao kuchunguzwa. Hakuna mtu anayeweza kuwaita wabunge wapuuzi kama hawafanyi upuuzi.
Elisa Muhingo
0767 187 507
   --

  

   Send Emails to wana...@googlegroups.com

  

    

  

   Kujiondoa Tuma Email kwenda

  

   wanabidii+...@ googlegroups.com 

  Utapata Email ya

   kudhibitisha ukishatuma

  

    

  

   Disclaimer:

  

   Everyone posting to this Forum bears
the sole

  responsibility

   for any legal consequences of his or
her postings,

 and

  hence

   statements and facts must be presented
responsibly.

 Your

   continued membership signifies that
you agree to

 this

   disclaimer and pledge to abide by our
Rules and

  Guidelines.

  

   ---

  

   You received this message because you
are subscribed

 to

  the

   Google Groups "Wanabidii"
group.

  

   To unsubscribe from this group and
stop receiving

 emails

   from it, send an email to wanabidii+...@
googlegroups.com.

  

   For more options, visit

  https://groups.google.com/d/
optout.

  





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments