Uhamiaji huo, uangaliwe pia bila kutenganisha falsafa ya Nyerere ya Umoja na Usawa.
Dodoma kuwa katikati kulimaanisha pia (na sasa bado kunamaanisha) kudumisha usawa kwa wananchi wote wa Tanzania. Lengo sio watu wa nje, lakini kwanza maana nzima ieleweke na kukubaliwa na Watanzania.
Ukiangalia kwa undani dhana nzima ya usawa, utaunga mkono mara moja kuharakishwa uhamiaji wa kuifanya Dodoma Makao Makuu HALISI.
Umoja wa Watanzania hauwezi kuakisiwa na makao makuu yaliyoko PEMBEZONI.
Umoja wetu, unatakiwa kuwa na mwangwi wa KATIKATI na sio pembezoni. Picha halisi ya mvuto, ukizivuta pembe zote kuja katikati utaeleweka kwa wale walio na shaka baada ya NAFASI YA KATIKATI kupewa umuhimu wake, na umuhimu huo ni uhamiaji halisi wa katikati ya nchi hii kubwa kuliko zote za Afrika Mashariki.
Mengine yooooooote, yatafuata baada ya hili.
Umuhimu na dhima yake; raha yake na maana kubwa VITAJULIKANA baadaye kwa wale ambao hawawezi kuona maana hiyo leo hii.
Lililo muhimu ni kuondoa vikwazo vya kimawazo, kiutendaji au kimwili, kijamii au kielimu ili uamuzi huo sasa uwe halisi.
Kuhamia Dodoma kunaunga mkono dhana za Umoja na Usawa. Dhana mbili zilizomo katika Falsafa ya Nyerere.
Aldin
Prof. Aldin K. Mutembei (PhD)
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Kampasi ya Mwalimu J.K. Nyerere
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
+255 715 426 162+255 715 426 162 [Kiganjani] +255 715 426 162
b-pepe: kaimutembei@gmail.com Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>
Call
Send SMS
Add to Skype
You'll need Skype CreditFree via Skype
--------------------------------------------
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments