KUWA SALAMA KATIKA MASHAMBULIO KAMA LA PARIS
Nchi ya Ufaransa ilikumbwa na shambulio la kigaidi lililoua watu 120 , 80 ndani ya ukumbi wa burudani , wengine nje na karibu na uwanja wa mpira wa StedE De France .
Katika shambulio ndani ya Ukumbi wa Burudani magaidi waliojivika mabomu walijilipua katikati ya watu wengine walifyetua risasi huku wakitafuta watu wa kuwauwa zaidi .
Shambulio hili kwa hakika limetupa funzo na somo kubwa .
Je wewe ukikumbwa na shambulio au ukiwa eneo kama hilo ufanyaje ? Hizi ni njia rahisi zaidi za kuwa salama na kuokoa maisha yako na ndugu zako .
KIMBIA
- Toroka toka eneo la tukio kama unaweza
- Fikiria Njia nyepesi zaidi itakayokuweka salama
- Je kuna njia salama ? Kimbilia huko au Jifiche
- Je unaweza kufika sehemu salama bila kujihatarisha ?
- Washawishi wengine waende na wewe
- Uchukue tahadhari miongoni mwenu anaweza kuwa gaidi
- Acha vitu vyako nyuma kama laptop , mikoba
JIFICHE
- Kama huwezi kukimbia , Jifiche
- Jifiche kutoka kwenye eneo lenye mapigano ya silaha
- Kama huwezi kumuona mshambuliaji , yeye anaweza kukuona
- Kujificha asikuone haimaanishi upo salama , Risasi zinapenya ukuta , vioo , mbao hata bati
- Unapojificha hakikisha uko eneo ambalo ni gumu risasi haiwezi penya
- Kuchukua tahadhari na njia ya kutokea
- Jitahidi usibanwe popote
- Kuwa Kimya , weka simu Silent
- Jifungie ndani , weka hata vitu vya kuongeza uzio
- Kaa mbali na mlango au madirisha
ZUNGUMZA
Piga simu Polisi - Polisi wanaweza kuhitaji yafuatayo
- Mshambuliaji yuko eneo gani ?
- Mara ya mwisho ulimwona wapi gaidi ?
- Muelezee Mshambuliaji , idadi yao , Nguo , Silaha , Alivyo ETC .
- Wahanga - Idadi yao , aina ya majeraha , Maelezo kuhusu Nyumba walipo , Milango ya kuingia na kutoka , Mateka .
- Wazuie watu kuingia katika Jengo hilo kama ni salama kufanya hivyo .
POLISI WAKISHAFIKA
- Fuata maelezo ya Polisi
- Kuwa mtulivu
- Unaweza kwenda katika eneo salama ?
- Usihame kwa Ghafla kitu kinachoweza kuwa hatari
- Weka mikono sehemu inayoweza kuonekana
POLISI ANAWEZA KUFANYA YAFUATAYO
- Kukuelekezea Bunduki
- Kukutibu au kukuhudumia vizuri
- Kukuhoji
- Wakati mwingine hawezi kukutofautisha wewe na mshambuliaji
- Polisi anaweza kukutoa eneo hatari pindi kunapokua na usalama
USIJIFANYE UMEKUFA
LAZIMA UWE SALAMA
- Una panga nini linapotokea tukio kama hilo au mengine ?
- Lazima uwe na mpango / mipango ya jinsi ya Kuepuka ila ni suala la kujifunza , kuchukua tahadhari na kuuliza maswali
YONA FARES MARO
0786 806028
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments