[wanabidii] Chonde Spika Mtarajiwa Ndugai; Usianze Kwa Kufufua Mjadala Uliouzika Mwaka 2012; Ni Wa Nyongeza Za Posho Za Wabunge..

Monday, November 16, 2015


Ndugu zangu,

Hata baada ya kumpongeza Spika mtarajiwa Job Ndugai kwa kupitishwa na chama chake kuwania Uspika, nataka niwe miongoni mwa wa mwanzoni kumtahadharisha Job Ndugai na kile ambacho baadhi ya Wabunge watapenda kusikia kutoka kwake. Ni heri achague kuchukiwa na wabunge kwa kuwaambia ukweli kuliko kuchagua kupendwa kwa gharama za wanyonge walio wengi. Watanzania katika hali ngumu ya kiuchumi kwa sasa, hawatarajii kabisa kusikia habari za Wabunge kuongezewa posho na marupurupu mengine, badala yake mijadala ya walau kupunguza posho zao za vikao ili fedha zitakazopatikana ziende kuboresha huduma muhimu za kijamii kama vile afya na elimu.

Na hapa nitamkumbusha Job Ndugai alichokisema mwaka 2012. Kwenye gazeti Uhuru Jumanne, Februari 7, 2012, limebeba habari hiyo kwenye ukurasa wa kwanza.

Mwandishi Lilian Timbuka akiripoti kutoka Dodoma alimnukuu Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akitamka; " Nyongeza ya posho ya vikao vya bunge sasa haitalipwa mpaka hapo Ofisi ya Rais, Ikulu, itakapotamka vinginevyo. Kwa kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuidhinisha vibali vya nyongeza za malipo kwa wabunge, ikiwemo posho na hajatoa kibali, hivyo haina haja ya kuendeleza mjadala kuhusu hoja hiyo"- Job Ndugai, Uhuru, Jumanne, Februari 7, 2012.

Maggid,

Dar es Salaam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments