[wanabidii] Kamwe Zanzibar Hakuna Atakayepata Ushindi Wa Kishindo..!

Friday, October 23, 2015


Ndugu zangu,

Pichani nikiwa mitaa ya Mji Mkongwe, Mwezi Februari 2010. Naongea na mmoja wa vijana wa Kizanzibar.

Nimeanza kufuatilia siasa za visiwani tangu nikiwa shule ya msingi. Na safari yangu ya kwanza kuvuka bahari ilikuwa ni kwenda Zanzibar mwaka 1988, mara tu baada ya kumaliza Form Four pale Tambaza Sekondari.

Ndugu zangu, 
Kazi ya kujaribu kuuelewa mfumo wa kijamii na kisiasa katika Zanzibar si kazi nyepesi.

Mfumo wa kisiasa katikaZanzibar kwa kiasi kikubwa unatokana na mfumo wa maisha ya Wazanzibar. Kuna historia, na siku zote historia ni mwalimu mzuri.

Tafsiri ya matukio ya kisiasa katika Zanzibar unaweza kuipata kwa
kuuangalia kwa karibu mfumo wa maisha wa watu wa visiwani. Inakutaka
usome kwa bidii, lakini zaidi ufanye bidii ya kuongea na Wazanzibar
wenyewe. Mara ya kwanza kufika Zanzibar ilikuwa ni Januari mwaka 1988.

Tangu hapo shauku yangu ya kutaka kuyajua ya visiwani iliimarika zaidi.
Kuna baadhi yenu huenda hamjui, kuwa kihistoria na kutokana na mfumo wa maisha ya Wazanzibar, kamwe hakuna chama cha siasa kinachoweza kupata ushindi wa kishindo.

Historia inatufundisha, kuwa Zanzibar imegawanyika mara mbili; Pemba na Unguja. Na nguvu za CCM na CUF katika visiwa hivyo zimejengeka katika misingi ya ZNP- ZPP na ASP.

Wakati Pemba ZNP-ZPP walikubalika kwa asilimia 55 asilimia 45 ilibaki kwa ASP. Na Unguja wakati ASP walikubalika kwa asilimia 65 , zilizobaki 35 ni za ZNP- ZPP.

Hali hii ilionekana kuanzia uchaguzi wa 1957. Na kimsingi imeendelea kuwa hivyo kwa chaguzi zilizofuata. Maana tunaona hapa kitakwimu, kuwa kwenye chaguzi za 1957, ASP ilishinda kwa 60.1 na ZNP na vyama vingine vikapata 38.2.
Januari mwaka 1961 ikawa ASP 40.2 ZNP na vyama vingine 52.8
Juni 1961 ASP 50.6 na ZNP na vyama vingine48.7
Mwaka 1963 ASP walipata 54.2 na ZNP na vyama vingine 44.6..

Kwa kuangalia mfumo huo, unaona, kuwa CCM na CUF Zanzibar wamekuwa wakichuana na pattern hiyo hiyo hadi hii leo.

Nachelea kusema, kuwa CCM Zanzibar wana faida ya kuwa upande sahihi wa historia hata kwenye uchaguzi wa kesho kutwa Jumapili.

Ndugu zangu wajumbe wangu kutoka Zanzibar, akina Sultan A Sultan na wengine, nakaribisha michango yenu...

Maggid,

Iringa.

http://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments