Ukawa bado upo chadema wanalitumia neno hilo kuombea kura? Nishawishini
Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) unaojumuisha vyama vinne vya CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD ulianzishwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba(BMK) kwa kile kilichodaiwa ni kutetea maoni ya Wananchi kwenye rasimu ya Katiba, maoni yaliyotokana na tume ya Jaji Joseph Sinde waryoba kama mwenyekiti wa tume hiyo.

Waasisi wa UKAWA walikuwa ni Mwenyekiti wa CUF wakati huo, Prof. Harouna Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, mzee Makaidi ambao waliongoza mapambano ndani ya BMK huku Makatibu wakuu wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD wakiongoza mapambano nje Bunge Maalum la Katiba.
Kati ya wenyeviti wa Vyama vinavyounda UKAWA, tayati watatu wamekosa uhalali wa kuwaaminisha watanzania kuwa wanapigania UKAWA. Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Lipumba yeye mwenyewe alijitoa kwenye umoja huo na kwenye chama chake kwa madai ya makubaliano ya UKAWA kukiukwa.

Mwenyekiti wa NLD, Mzee Makaidi haeleweki tangu wapiga kura wa jimbo la Masasi walipomkataa mbele ya Mgombea mwenza wa UKAWA, Juma Duni Haji. Mzee Makaidi haijulikani siyo tu kama ana wanachama bali hata uongozi wa chama na ndiyo maana baada ya kukataliwa kule masasi, habari za NLD zimetulia kama maji ya mtungi.
Hivi karibuni Makamu mwenyekiti na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi wamejitokeza hadharani na kumshutumu Mwenyekiti wao , James Mbatia kuwa amekiua chama kwa kujifanya msemaji wa CHADEMA n.k.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na mpambanaji wa UKAWA nje ya Bunge maalum la Katiba, Dr. Wilbrod Slaa naye hayuko na chama chake.
Kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu zinaendelea huku kukiwa na sintofahamu kubwa ndani ya UKAWA. makubaliano ya kuachiana wagombea udiwani na Ubunge ndani ya Umoja huo yamekiukwa kwa asilimia kubwa, mbaya kabisa Majimbo ya wenyeviti wenza wa UKAWA ambayo yalitakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza makubaliano hayo nayo yana mgogoro.

Jimboni kwa Makaidi wapiga kura wamemkataa kama mgombea Ubunge. Jimboni kwa Mbatia madiwani wa CHADEMA wameapa kutompigia kampeni kwa madai ya kukiuka makubaliano na kusimamisha wagombea udiwani katika kata zote 16 za jimbo hilo.
Kwenye kampeni za urais huoni bendera ya CUF, NCCR wala NLD ikipepea. Huoni kiongozi wa kitaifa wa NCCR, CUF wala NLD. Husikii salaam ya NCCR, CUF wala NLD.
NISHAWISHINI, BADO KUNA UKAWA AU UMEBAKI UKAWA WA KUPELEKA CHADEMA IKULU BASI?
NISHAWISHINI, BADO KUNA UKAWA AU UMEBAKI UKAWA WA KUPELEKA CHADEMA IKULU BASI?
0 Comments