Mda wa mafuriko na Tsunami umeshapita sasa ni muda wa midahalo!
Baada ya kutambiana hapa na pale sasa ni wakati muafaka kama Taifa tukashinikiza midahalo ya wagombea.
Jambo hili sio jipya kwani wakati Mkapa anagombea kulikuwa na mdahalo kama sikosei Masako na Pasco walivuma sana kipindi hiki kwa kutuletea midahalo ya wagombea kama vile Mrema ,lipumba na Mkapa.
Mwaka 2010 mzee makamba alikataza makada wa ccm kuingia kwenye midahalo.
Mwaka huu kinana ameruhusu wana ccm kuingia kwenye mdahalo.
Bahati mbaya sana ukawa wanataka kutuuzia mbuzi kwenye gunia eti wanataka mdahalo wa wenyeviti!!utadhani wenyeviti ndio wanaomba nafasi za kutumikia serikali!
Nataka kuona Ukawa wakiweka 'drones' kwenye studio za TBC/ITV ili kurusha live Tsunami na Mafuriko ya hoja.
0 Comments