Fumbuka na wengine…!!!!
Nafikiri tunahitaji toba!! Toba ya kweli kwa Mungu wetu na mbele ya watu wetu. Hii inatokana na ukweli kuwa tumekuwa watu wazito kusema "hapana" kwa kile tunachokiamini na kulazimisha wengine wakubaliane na kile tunachokiamini kwa hoja nyepesi kabisa. Watu tulioaminika kuwa ni Public Intellectuals tumefika mahali tunaisaliti jamii yetu!!!? [Wasomi kizimbani?!!] Tumenaswa katika mikoba ya uchawi wa Giningi na kusahau kabisa uganga (Udaktari) ambao tumeusomea na kufuzu kwa viwango vilivyotukuka. Historia itatuhukumu!. Nakumbuka 2007 , usiku mmoja katika kumbukizi/tafakari ya maisha ya marehemu Prof. CSL Chachage niliwaeleza wanazuoni waliokusanyika kwa ajili ya tukio lile kuwa jamii yetu ipo katika kitu inaitwa " apocalyptic moment". Hali tata inayodhihirisha fumbo la maisha yetu . Fumbo hili ni kwamba, kuna pengo kubwa kati ya ukweli wa maisha yetu na jitihada za mantiki tunayotumia ili kuona ukweli huo . Unaweza kujisomea zaidi kwa kubonyeza HAPA
Hakika nimepata shida kidogo kipindi hiki.Nimelazimika wakati mwingine kushinda maktaba kujaribu kujiridhisha juu ya baadhi ya watu na michango yao hapa jukwaani na kuishia kufedheheka tu.Mfano mzuri ni mama NKYA!! Nimefanikiwa kupata makala zake za kutosha tu tangu 2010 hadi sasa.Yeye ni mmoja wa wale wanaohitaji TOBA kwa kweli.Kimsingi tumesahau wajibu wetu kwa jamii yetu, na historia itatuhukumu.
Kazi ya mja kunena.
______________________________
Without "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
______________________________
A D D R E S SWithout "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
______________________________
John J. Malata
Secretary General,
Society Empowerment Agency
Mobile: +255 782366090
0 Comments