Bulaya alikoroga Bunda
UAMUZI wa vikao vya juu vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwapitisha wagombea ubunge bila ridhaa ya wanachama huenda ikaathiri mwenendo wa uchaguzi katika Jimbo la Bunda.
Taarifa kutoka jimboni humo zinasema kwamba uteuzi wa Esther Bulaya aliyeanguka kwenye kura za maoni jimboni humo, umekipasua chama hicho baada ya viongozi wote wa juu jimboni humo kusimamishwa kazi na baadaye kutangaza kuachia madaraka.
Esther alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kabla ya kuamua kukimbilia Chadema ambako aliangushwa na kada wa upinzani Bunda Mjini, Pius Masururi, lakini akarejeshewa kijiti cha kugombea jimbo hilo na Kamati Kuu ya Chadema.
Akizungumza na Radio Mazingira FM ya mjini hapa juzi muda mfupi kabla ya kuelekea Nairobi, Kenya, Masusuri alisema ameachana na Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Nimeshindwa kuvumilia uonevu huu na ninawaomba wote waliokuwa wakiniunga mkono Chadema, kumpigia kura
Wasira (mgombea wa CCM, Stephen)," alisema Masusuri na kuongeza:
"Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman) huwa anasisitiza kuwa asiyefanya kazi na asile. Sasa inakuaje mimi niliyeanza kulitengeneza jimbo hili tangu mwaka 2013 leo niachwe, achukuliwe ambaye hajakifanyia chochote chama?
"Mwanachama mwenye wiki moja tu hata mkutano mmoja wa hadhara hajahutubia leo anapewa nafasi kubwa kuliko sisi!"
Tayari wana Chadema saba wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Masururi nao wamejiunga na CCM jana.
Chadema iliwasimamisha uongozi Mwenyekiti wa Jimbo la Bunda, Samwel Imanani; Katibu Mwenezi, Emmanuel Malibwa na Katibu wa Wilaya, Rita Tosile ambao pamoja na madai mengine, wanatuhumiwa kutumiwa na CCM kukidhoofisha chama hicho.
Taarifa za kusimamishwa kwao zilithibitishwa na Katibu wa Jimbo la Bunda, Daniel Charles.
Hata hivyo, wanachama wa Chadema waliokuwapo ofisi za chama hicho jana waliliambia Raia Tanzania kuwa wanaunga mkono hatua ya Makao Makuu kuwasimamisha viongozi wao.
"Hata Masusuri mwenyewe, tulishamshitukia muda mrefu kuwa anatumiwa na Wasira, kwa hiyo bora alivyoondoka," alisema mwanachama mmoja akionekana dhahiri kumuunga mkono Esther.
Baadaye, kiongozi mmoja aliyesimamishwa na baadaye kuamua kuachia ngazi, Rita, alidai kuwa Masururi alionewa na kwamba sasa Chadema wajiandae kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu.
"Nimeachia ngazi kwa kuwa ninajua chama hiki sasa kitashindwa kwenye uchaguzi. Sasa makamanda waliokipigania chama kwa muda mrefua wanaachwa, badala yake wanakuja wageni.
"Uongozi wa taifa unapasawa kuheshimu uamuzi wa wananchi waliompa ushindi wa kwanza mgombea kwenye kura za maoni ni si vinginevyo," alisema Rita.
Sarakasi Jimbo la Mbarali
Wakati hali ya Bunda ikiwa hivyo, Mwandishi Wetu kutoka Mbarali mkoani Mbeya anaripoti kwamba makumi ya wananchi wilayani humo jana walizingira Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya (DED) wakishinikiza Modestus Kilufi apewe fomu za kugombea ubunge.
Kilufi ni Mbunge anayemaliza muda wake ambaye ameondoka CCM na kujiunga na Chadema hivi karibuni na kisha kupewa jukumu la kutetea nafasi yake Mbarali.
Lakini kabla hajakwenda Mbarali, uongozi wa Chadema Wilaya ulimwandikia barua Msimamizi wa Uchaguzi wilayani humo ambaye pia ni DED, Adam Mgoi, kumtambulisha Laurent Mwang'ombe kuwa ndiye mgombea ubunge na kuchukua fomu hizo juzi.
Jana, Mwang'ombe alikula kiapo mahakamani na wakati akijiandaa kuzirejesha fomu zake, ndipo msafara wa Kilufi aliyeongozana na viongozi wa Chadema Mkoa ulipowasili wilayani humo na kwenda moja kwa moja ofisi za Chadema.
Alipowaona wageni hao, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbarali, Peter Mwashiki, alilazimika kuikimbia ofisi huku wanachama wakimkimbizi na kumtaka kumpeleka Kilufi kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
Baada ya kushindwa kumpata Mwasiki, Kilufi akiongozana na makumi ya wanaChadema, walikwenda ofisini kwa DED lakini nako waligonga mwamba kwani msimamizi huyo aliamua kufunga ofisi akiwaacha nje wafuasi wa Chadema, Kilufi na uongozi wa mkoa.
"Wananchi wanamtaka Kilufi agombee ubunge kwani hawana imani na Mwang'ombe. Wanadai kuwa huyu amefanya mipango na mwekezaji (shamba la mpunga lenye mgogoro na wananchi) ilia je kumlinda baadaye," walisikika wananchi wakimlalamikia DED.
Hata hivyo, ofisi za NEC ambazo zipo chini ya Mgoi hazikufunguliwa hadi jana jioni huku wananchi wakiapa kutoondoka eneo hilo hadi 'kieleweke'.
Raia Tanzania

0 Comments