Na Ahmad Mmow, Lindi
· BODA BODA WAPINGA JARIBIO LA KUTAKA KUDHULUMIWA UJIRA WAO
· WALIAHIDIWA MAFUT LITA, 3 NA SH. 10000 KILA MTU KWA SAA MOJA
· MKUU WA MKOA WA ZAMANI ATOA ZAKE MFUKONI KUZIMA HASIRA
Fedha zinazohusishwa moja kwa moja na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowasa, katika safari yake ya kuelekea ikulu aliyoipachika jina la ''Safari ya Matumaini'' zimezua balaa baada ya waendesha pikipiki, maarufu kama bodaboda, takribani 70 kuingia mzozo wa namna ya kulipwa ujira wao.
Kiini cha mzozo cha huo ni kukiukwa kwa makubalianao ya awali kati ya mratibu wa mapokezi ya Lowasa kutoka uwanja wa ndege wa Kkwetu (Lindi) hadi ofisi ya ccm mkoa, amabaye aliwaelza waendesha bodaboda hao kwamba watawekewa lita tatu za mafuta kwenye pikipiki zao na kila mmoja atalipwa ujira wa shilingi 10000 kwa kazi itakayodumu kwa saa moja tu.
Hata hivyo, kinyume cha makubaliano hayo, Lowasa alichelewa kutua uwanja wa ndege kwa zaidi ya saa tano na hiyo, bodaboda hao kuingia makubaliano mapya na mratibu huyo, wakitaka walipwe shilingi 20000 yaani nyongeza ya shilingi 10000.
Wakizungumza na Raia Tanzania kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazeti ili kuepuka visasi dhidi yao , baadhi ya waendesha bodaboda hao walidai mratibu huyo, kwa kushirikiana na waendesha bodaboda mashabiki wa Lowasa walikubali wenzao walipwe nyongeza hiyo ya shilling 10000.
"Baada ya makubaliano hayo, tulifanya kazi yetu vizuri sasa tatizo likaibuka katika malipo,ilibidi tuongozane hadi ofisi ya ccm ili kudai haki yetu na huko tuliambiwa ccm haihusiki wakatushauri twende polisi. Tulikwenda polisi na Yule (mratibu) aliyetuahidi tutalipwa pesa. Tulimpakia kwenye bajaji lakini baadaye tukiwa njiani gari za polisi zilitufuata na kumchukua na kumweka ndani kwa ajili ya usalama wake".
"RPC (mkuu wa Polisi mkoa wa lindi) alituambia tunayo haki ya kudai chetu kwa kuzingatia makubaliano, wakati tukiendelea akatokea Abdulaziz (mkuu wa mkoa wa zamani wa lindi) na mbunge wa Lindi Mjini) akatuchukua na kutupeleka kwenye stationary ya mfanyabiashara mmoja anaitwa Ali Nalenga"
"kwa kuwa tulikuwa tumeorodheshana majina, alikuwa akiita jina mmoja baada ya mwingine na kutulipa 15000, unajua baada ya ugomvi tulitaka kulipwa shilingi 40000 lakini akatupa 15000" alisema mmoja wa waendesha boda boda hao.
Habari kamili tafuta Raia Tanzania (ijumaa june 19, 2015)
0 Comments