[wanabidii] Neno 'UFISADI' limekuwa chungu mdomoni mwa viongozi wa CHADEMA

Wednesday, August 26, 2015
Neno 'UFISADI' limekuwa chungu mdomoni mwa viongozi wa CHADEMA
 
    Katika chaguzi zilizopita, CHADEMA walikuwa jasiri kutamka hadharani bila woga na kwa kujiamini. Walikuwa wanatamka kuhusu CCM kuwa chama cha mafisadi. Naam, neno fisadi lilikuwa taam mithili ya Halua ama Asali kwa wale wasiojua Halua. Kuanzia kiongozi mdogo mpaka mkubwa wimbo ulikuwa mmoja tu. CCM ni chama cha mafisadi.
    Sasa upepo umegeuka. Ni baada ya kufanya makosa ya kupokea makapi yaliyotemwa CCM kutokana na kashfa za ufisadi. Naam. Fisadi kawa mgombea wa CHADEMA na UKAWA. Tena fisadi amekuwa mfadhili wa uchaguzi wa mwaka huu .
    Kwa sasa CHADEMA wameambiwa na Lowasa, shut up your mouth.

Hakuna kutamka neno fisadi. Na kweli wote wapo kimyaaaa! Wamegwaya na wamenyamazishwa na fisadi. Kwikwikwikwikwikwikwiiiiiii! Akina Mbowe nao wamegeuka kuwa mafisadi baada ya kuuza chama kwa bilioni 10.
    Sasa neno fisadi limekuwa chungu mithili ya shubiri. Naam, waweza pia kusema kuwa imekuwa chungu kama mwarobaini kama hiyo shubiri huijui.

Share this :

Related Posts

0 Comments