[wanabidii] Lowasa tembelea na huku

Wednesday, August 26, 2015
Naamini Mheshimiwa Lowasa utatembelea kwenye jela za Keko na Segerea
 
   
 
    Mheshimiwa Lowasa jana ameingia siku ya pili katika ziara zake za kuwatembelea wananchi ili kujua matatizo yao then aweke mikakati ya kuyatatua endapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi. Nampongeza sana kwa hatua hiyo kwani chama chake cha CHADEMA hakina Ilani ya kumnadi mgombea wake ndipo Lowasa alipochanganya akili za kuambiwa na zake.

    Juzi alikuwa Gongolamboto, Chanika na Mbagala. Jana alikuwa maeneo ya Manzese, Tandale na kwingineko. Naamini kuwa safari zake zina mafanikio kwake hasa baada ya chama chake kupoteza mwelekeo.

    Pamoja na pongezi hizo, natoa wito kwake. Katika ratiba zake za kuwatembelea wananchi, asisahau kutembelea jela zetu. Sehemu muhimu kwake ni Segerea, Keko, Ukonga na kwingineko. Naamini kuwa kwenye hizo jela kuna Watanzania wengi ambao Lowasa anaweza kuwasikiliza na kupata changamoto zinazowakabili.

Muda mzuri wa kukaa na wafungwa ni usiku ambapo wafungwa wengi wanakuwa wamejipumzisha na hapo ndipo Mheshimiwa Lowasa anaweza kutumia fursa hiyo kuzungumza na wafungwa hao. Naamini kuwa akitoka hapo akili yake itakuwa sawa na ari ya kuomba kura kwa wananchi itaongezeka.
    Ni ushauri tu nampa Mheshimiwa Lowasa. Maadam ameamua kuwatembelea wananchi wote, basi asisahau kuwatembelea na wafungwa kwenye selo zao

Share this :

Related Posts

0 Comments