[wanabidii] Mdahalo kati ya POLEOLE NA MSIGWA ULIVUOKUWA CHANEL TEN

Tuesday, August 11, 2015
POLEPOLE
UKAWA imebadilisha malengo, nchi hii imechoshwa kuongozwa na watu wenye madoa, Afrika haiendelii kwa sababu ina watu kama hawa na haiendelee. Nkawaambia CCM kama itaendelea na watu wenye madoa wasanifu ambao kwa kuwepo kwao inaambukiza na wengine.

Nikasema nitapiga kelele wasichaguliwe na kweli wakakatwa, sasa mmoja kaenda UKAWA na huyu akichaguliwa atakua rais wa watanzania na si rais wa wanaUKAWA. Tangu 95 alikuwaanataka kuwa rais, Mwinyi alimshitaki huyu kwamba hafai, Mtu mwanaume Malaya anastahili kuwa kiongozi?

Mtu huyu hafai kuwa kiongozi wa taifa letu kwa sababu ya maadili na huwezi kusema tunasuburi mahakama ithibitishe.

Tukikuuliza utajiri umepata wapi unasema unachukia umasikini. Unasema zimetoka kwa marafiki, kwa kipi!

Leo hii mnakuja huyu mtu ni msafi kwa sababu hakwenda mahakamani, legitimacy ni jinsi unavyoishi, huwezi kwenda Ikulu kwa kukiuka misingi na maadili, my problem is this guy have so much to answer, mimi ni raia na nina haki ya kuhoji, nimekuwa mstari wa mbele kuipigania katiba, mchungaji haiwezekani wewe umetee mtu ambao ni mchafu kwa kigezo kwamba hajapelekwa mahakamani.

MSIGWA
Hapo unapozungumza najua ushahidi hauna, nikikuzungumzia wewe pia utasema ushahidi hauna! Wakati wewe unaenda bunge la katiba, walikwambia ujiuzulu kwanza kwa sababu kazi ni ya full time na ukagoma na bahati mbaya ulipoondoka na taasisi ikafa, TYC mlikuwa mnashirikiana na DANIDA, kuna laki sita zilipotea pia kuna taarifa kwamba ulikuwa unawataka wanawake kwenye taasisi yako(Kaambiwa arudi kwenye mada)

UKAWA tulilalamika, na alichofanya Polepole kutetea katiba ulikuwa ni wajibu wake kwa sababu alikuwa , kwenye list of shame tulimtaja JK lakini mbona Polepole hamtaji JK.

Yukisema tuwahuku watu kwa tuhuma tutakuwa tunawaonea. Lowassa ameondoka kwenye chama cha mafisadi na sasa yuko kwetu, katika watu ambao ninaweheshimu ni Lowassa kwa sababu kaambiwa mengi lakini amekaa kimya.

Hatukukurupuka kumleta Lowassa, mimi kama mkristo, yeye ambae hana dhambi aanze kumruhie jiwe, hata kama kweli Lowassa ni fisadi amekuja kwenye UKAWA. Jamii inaona kwamba unatumiwa kwa sababu hujamzungumzia Magufuli, katudanganya kuhusu barabara na wizara yake imetuhumiwa na CAG.

Unasema Lowassa ana mapesa mengi sijui kama unajua akaunti za Lowassa, huwezi kuthibitisha. Humtaji mgombea mwenza wa Magufuli kuhusu katiba ya wananchi, yesu alisema yeye ambae asie na dhambi aanze kumrushia mawe. Wengine wanasema sisi tulikuwa tunamsema, its true hata mimi nilimsema, kwenye politics kuna pande mbili ambazo zinakinzana.

POLEPOLE
Mimi ukiniita hapa, nakuja kuongelea hoja ambayo wewe umeiweka mezani tofauti na mimi ningekuita labada kwangu au hotelini ningekueleza ninachotaka kuzungumza, hivyo mheshimiwa Msigwa mimi nazungumza hoja ambayo imewekwa mezani na si mimi nnaechagua.

Mimi nilipata bahati kufanya kazi katika asasi za kiraia, baadae nikapata dhamana ya kuwa mkurugenzi wa TYC, baadae nilikuja kustaafu na niliicha vizuri na mpaka leo ipo mtaa Agachube nyumba namba 127, nilistaafu japo kwenye asasi hizi watu hawastaafu, 2011 nilichaguliwa na asasi za kiraia kuwa mwenyekiti wa asasi zote za kiraia nchini, mimi ndie nilichukua maoni ya wananchi na kwenda kumuona rais na kusema haya ni maoni ya wananchi. Book lile ndilo lilitotumika kurekebisha sheria.

Niliandika barua ya kujiuzulu japo niliambiwa na Sophia Simba niendelee, Unasema nimegombana na DANIDA, DANIDA miezi mitatu iliopita wameniita mimi wakasema tusaidie kazi hii ya mshahara mnono. Msigwa amelishwa maneno asiyoyafahamu.

Kuna watu wanasema mimi natumiwa, tumesimama kidete kusema maneno ya wananchi, Msigwa nikueleze nimewasema CCM muda mrefu mpaka wakasema nyie wapinzani mnanilipa pesa ili niwaseme wao, sasa nikuulize Msigwa mlinipa shilingi ngapi?. Msigwa wewe humjui Lowassa, mimi namjua akiwa ndani ya CCM.

Ametoa maoni tume kwamba mimi nataka serikali tatu, nikachukua masaa mawili kumuelezea rasimu, baadae akasema yeye anataka muungano wa serikali mbili, nikamuuliza wewe si umesema unataka serikali tatu, anataka serikali ambayo uhusiano na Zanzibar ni defence tu, huyu anataka kuvunja muungano

SIMU(MASWALI)

  1. Mchungaji kafeli anatetea vitu vya ovyo
  2. Kaijage: Kwanza nimpongeze Polepole, nadhani UKAWA wamekosa mtu wa kujadili na Polepole, watu ambao wametumia miaka minane kumsema Lowassa ni fisadi ni hawahawa CHADEMA, leo hii wana kazi kubwa sana ya kumsafisha
  3. Wabaki kwenye mada maana kunyooshea vidole wao kwa wao haitusaidii, wabaki kwenye mada
  4. Wakati Lowassa anatuhumiwa ni fisadi, 2008 CHADEMA walisema ushahidi wanao Mwembeyanga na anaeona kaonewa aende mahakamani, namuuliza Msigwa ushahidi bado wanao?
  5. Upande wa Lowassa kachemka huyo
  6. Sikutegemea, Humprey kapanic, mnaongelea mambo ya familia na mambo binafsi ya Lowassa, tulikuwa tunataka hoja nzuri za kujenga hii nchi
  7. Songo(Bukoba): Nimpongeze mchungaji Msigwa, huwezi kumtuhumu mtu bila ushahidi
  8. Rahim: Nimpongeze Msigwa, tunamuelewa pia nimpongeze Lowassa, ni mtu jasiri.
  9. Nakupongeza kwa vipindi unavyondesha lakini kwa kipindi hiki cha uchaguzi naomba visiwe live maana kuna watu wa CCM na UKAWA wanatetea watu wao, maana nakuonea huruma jinsi unavyowatenganisha Polepole na Msigwa, watu tuna presha na vyama vyetu, kuna watu hapa nyumbani wanabishana kwa ajili ya vyama vyako kutokana na kipindi hiko.
  10. Nampongeza Polepole kwa kulenga kwenye mada ila huyu mwingine anaenda nje, Lowassa ana madoa na kama umejitokeza mahali kama hapo uvumilie
  11. Polepole amekosea, angeuliza kwanza kosa la Lowassa ndio aje kujengea hoja
  12. Nimefurahi sana mada yako lakini mchungaji anaonekana anamtetea Lowassa badala ya taifa, sisi hapa tuna lengo la maslahi ya taifa sio kuiondoa CCM
  13. Lowassa aliamua kukimbilia UKAWA baada ya kuona fursa ndani ya CCM haipo tena, wao ndio wamemtuhumu Lowassa kwa miaka nane, walisema wakati tuko Dodoma kwamba tuko huko kujaribu kumbakisha fisadi mwenzetu Lowassa, sioni dhamira ya dhati ya Lowassa na mabadiliko ya kweli.
MSIGWA
Nadhani natakiwa kujibu mengi kuliko Polepole, kuna mtu kasema tulikuwa tunamsema Lowassa kwa miaka nane. Dhana ya kumsafisha imetoka CCM, tunamsafisha kwa kosa gani, mtu ambae Dar shughuli zimesimama tumsafishe kwa lipi, kwanini asisafishwe Magufuli ambae hakuwa ana watu wakati wakati wa kuchukua fomu.

 Kama tulimsema alafu tulikosea haina maana haiwezi kubadilika, Lowassa hajakuwepo kwenye serikali ya CCM kwa miaka nane. Tunachosema sio haki kusema yeye ndio mwiiiizi kuliko wote ndani ya nchi na hatuna muda wa kumsafisha na poll inasema watanzania wanaoshughulishwa na ufisadi ni asilimia tano (5%) tu. Watanzania sasa hivi wanataka change hawajali nani analeta, ndio maana unakuta kuna watu wanajizulu siku mbili wameshasahauliwa, hali iliyotokea jiji la Dar haijawahi kutokea

POLEPOLE
Mchungaji amesema nyinyi watanzania mnataka mabadiliko na atakaeleta yeyote nyie hamjali.
Mnasema mnataka kuitafuta pepo kwa namna yoyote hata kwa kupiga tunguli. Watanzania sio fanatics, sio wanazi tena akitoka hapa aite wandishi awaombe radhi kwa watanzania. Anasema watanzania wanataka ufisadi, kwamba hawajali kuhusu ufisadi. (Polepole ameondoa hoja yake baada ya Msigwa kugoma).

 UKAWA nina mapenzi nao ya dhati, napata ugumu kuicha inapokosea, CCM wakikosea huwa nakula nao sahani moja. UKAWA wenzangu tulishughulika na katiba ya Warioba, dhana kwamba Lowassa akija atafata UKAWA, mkumbuke Lowassa akiwa Rais kwa katiba ya 1977 ambayo atakuwa mamlaka karibu na Mungu mtu, mnafikiri akipata Urais atawajali nyie UKAWA au rafiki zake wa siku nyingi, nyie ni basi tu la kumfikisha Ikulu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments