Makapi ni uchafu unaotokana na kitu chenye uasili wake. Mara nyingi, makapi yaakishatolewa kutoka kwenye uasili wake, kinachobakia katika asili yake halisi (original).
Mara nyingi makapi hutokna na vykulula na kila aina ya chakula kina aina yake pia ya makapi. Kwa mfano wenyeji wa mikoa ya kaskazini inakoikwa na kunywewa pombe ya kienyeji aina mbege, makapi ya pombe hiyo huitwa machicha.
Hivyo hivyo kwa wakazi wa mikoa ya pwani mimea inayolimwa sana ni minazi, nazi zikishakamuliwa au kuchujwa na kupta tui la nazi kwa ajili ya kuungia mbog kama mbdala wa mafuta ya viwandani, makapi ya nazi yanayobakiwa na kutupwa huitwa machicha.
Mifano ya makapi ipo mingi kwa nchi zetu za kiafrika, makapi ni makapi tu yawe ya mpunga, mahindi,lizeti na kadhalika, hata chakula kinachobakizwa baada ya kula wakati mwingine huitwa makapi na sehemu ya kuhifadhi mkpi ni jalalani au kwenye shimo la taka.
Kwa hiyo, makpi aiana yeyote hayawezi kuwa chakula cha binadamu, ambayo ama yatatupwa jalalanoia au kufnywa chakula cha mifugo kama Mbuzi, Ng'ombe, kondoo, kuku, bata, ngamia nakdhalika.
Ndiyo kusema basi kwamba makapi, machicha aua pumba hata yajazwe kiasi gani, hayawezi kumuokoa mwanadamu anapokumbwa na njaa. Siku hivi katika siasa haswa katika kipindi hiki cha uchaguzi kuna msamiati mpya ulioibuka wa wanasiasa makapi, hawa ni wale waliopitishwa kwenye chujio la chama cha mapinduzi CCM, walitupwa nje na chjio hilo kwa kuonekna hawafai kupewa nafasi za uongozi kutokana na sababau mbalimbali na walea ambao walishindwa kupenya kutokana na ushindani uliokuwepo, baadhi yao wamejiondoa ndani chama hicho na kuhamia Chadema.
Viongozi wa chadema na ukawa kwa ujumla walililipokea kapi hilo la kwanza , Lowasa na kusikika kupitia vyombo vya habari kuwa lazima walitumie kapi hilo kuiondoa CCM madarakani. Wasichokifahamu ni kwamba makapi ni makapi tu, hata yajazwe kwenye ghala nkiasi gani hayawezi kuwa lilishe yeyote ya shibe kwa Mwanadamu mwenye Njaa.
0 Comments