[wanabidii] Dr nchimbi: "wanaonung'unika sasa ni wasaliti"

Sunday, August 16, 2015

Dr nchimbi: "wanaonung'unika sasa ni wasaliti"

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr Emmanuel Nchimbi amesema wale wote wanaolalamika hivi sasa kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ni WASALITI.

Dr Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati kuu ya CCM amesema watu hao ni walafi wa madaraka na ni watu ambao hawana nia njema na wananchi na kamwe hawawezi kuleta mabadiliko wanayoyahubiri.

Amesema katika mchakato wowote kama waliokuwa nao, ni kawaida kuwa naz makundi yanayowaunga mkono wagombea mbalimbali lakini kwa watu wastaarabu makundi hayo hufa mara mgombea mmoja anapopatikana. Dr Nchimbi ambaye wakati wa mchakato kule Dodoma alitoka nje na kulalamikia uamuzi wa kuondoa baadhi ya majina, amesema CCM iko IMARA na kwamba mgombea aliyeteuliwa na chama Dr John Pombe Magufuli ni mchapa kazi hodari atakayeiletea nchi maendeleo.

"Mkifanya uteuzi, yeyote anayepinga baada ya hapo huyo ni MSALITI," alisema na kuongeza..."Kipimo cha uaminifu wa mtu kwa chama ni wakati wa michakato migumu kama hii...hawa walioondoka wametudhihirishia kwamba hata wakati wakiwa ndani ya chama walikuwa ni wasaliti tu.."

Amemwagia sifa Dr John Pombe Magufuli kwa kusema ni mtu asiyekuwa na makuu na ndio maana wakati wa mchakato hakuwa na makundi kama wagombea wengine.

Dr Nchimbi alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la vIjana wa CCM jijini Dar es Salaam hapo jana.

Pia alimsifu Dr Magufuli kwa mchango mkubwa wa kufanikisha ujenzi wa jengo la UVCCM jijini Dar es Salaam wakati akiwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Share this :

Related Posts

0 Comments