Dowans wakubuhu wizi
Na Saed Kubenea - Imechapwa 05 January 2011
VIGOGO ndani ya serikali wanatuhumiwa kupanga njama za kutaka kuilipa inyemela mabilioni ya shilingi kampuni ya Dowans, kabla taratibu muhimu kuhitimishwa.
MwanaHALISI lina taarifa kuwa Dowans Tanzania Ltd., imewasilisha ankara zake Hazina, tayari kwa malipo kabla maamuzi kusajiliwa mahakama kuu.
Wakati taarifa hizo zikivuja, umetokea utata wa kampuni ipi hasa ya Dowans ilipwe, kwani kuna makampuni mawili yaliyojitokeza.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) ndiyo ilikuwa na mkataba na Tanesco kupitia kurithi mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond.
Bali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya Biashara (ICC) wa 15 Novemba 2010, unaagiza Tanesco kulipa Sh.185 bilioni kwa makampuni yote mawili.
Makampuni hayo ni Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Limited.
Utata huo unaongezeka kwa vile wakati wote wa mgogoro wa Richmond na Dowans, hakukuwa na Dowans Tanzania Limited ambayo sasa imetinga katika maamuzi ya ICC.
Nayo kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica), hata hivyo iliwahi kutajwa na msajili wa makampuni nchini Costa Rica kuwa haijawahi kusajiliwa nchini humo.
Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Dowans ni mradi wa vigogo watatu wakubwa ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka ndani ya serikali zinasema, mpango wa kulipa makampuni hayo unasukwa kwa ustadi mkubwa na watumishi wawili –mmoja kutoka wizara ya nishati na madini na mwingine ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG).
Alipoulizwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo kuhusu njama za kutaka kulipa Dowans kinyemela alisema, "Hapa ninapozungumza na wewe niko Kilosa. Sina taarifa za karibuni za ofisini." Mkullo alikana pia kujua iwapo Dowans wamewasilisha ankara kwa ajili ya malipo.
Kwa mujibu wa sheria za usuluhishi nchini na zile za kimataifa, uamuzi wa ICC sharti usajiliwe katika mahakama kuu ya Tanzania.
Aidha, kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo katika mkataba kati ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Tanesco, yote yaliyokubaliwa ndani ya mkataba yatafuata sheria za Tanzania.
Hata hivyo, taarifa zinasema, msukumo wa kutaka malipo hayo kufanywa kinyemela, umefuatia kutajwa katika mwenendo wa kesi, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
"Hapa kuna kitu kinafichwa. Rostam hataki kesi hii isajiliwe hapa, maana jina lake limetajwa ndani ya kesi hii zaidi ya mara tatu. Hivyo anajua kuwa iwapo itasajiliwa ataumbuka," ameeleza ofisa mmoja wa serikali.
Naye mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini amethibitisha kuwa ankara za madai ya Dowans tayari zimewasilishwa serikalini kwa hatua zaidi.
"Bodi ya Tanesco iliarifiwa jambo hili katika kikao chake kilichofanyika 21 Desemba 2010, na kila mmoja alishtuka," ameeleza mtoa taarifa.
Alisema, "…wanaleta ankara za madai hata kabla mahakama kuu haijasajili kesi yao? Hapana! Tukasema, sisi bodi hatuwezi kuidhinisha malipo haya…"
Kutajwa kwa Rostam katika shauri la Dowans kulifuatia kubanwa na majaji wa mahakama hiyo, mfanyakazi wake mmoja kutoka kampuni ya Caspian.
Mfanyakazi huyo aliyekuwa anahudhuria bila kukosa vikao vyote vya mahakama vilivyokuwa vikifanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, alieleza mahakama, "…niko hapa kufuatilia maslahi ya bosi wangu."
Mtoa taarifa anasema, "Yule bwana aliulizwa na wale majaji, mbona kila siku anaingia mahakamani na hatoki mpaka muda wa kesi unamalizika."
Anasema, "Ndipo yule kijana akajibu, 'nimetumwa na bosi wangukumwakilisha.'" Mahakama ikataka kujua huyo bosi ni nani? Ndipo akamtaja Rostam," anaeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.
Anasema mara baada ya kutaja jina la Rostam, majaji waliokuwa wanasikiliza shauri lile, haraka wakauliza, 'Kwani Rostam ni nani katika Dowans?' Yule bwana akajibu, 'Ni mwanahisa…'"
Kuna taarifa za kuaminika kuwa mmoja wa watu wawili waliosaini makubaliano ya kuhamisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans, ni Henry Surtees, Mwingereza anayedaiwa kuwa mtumishi wa kampuni ya Rostam ya Caspian.
Wiki iliyopita, gazeti la kila siku la Mwananchi lilimnukuu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema akisema, Dowans ilisajiliwa nchini Costa Rica na Rostam ndiye aliyepewa nguvu ya kisheria kusimamia malipo hayo.
Werema hakuzungumzia kwa undani hatua ya wanaojiita wamiliki wa Dowans kumpa Rostam nguvu hizo za kisheria.
Tarehe 7 Februari 2008, Rostam alikana kumiliki aina yoyote ya hisa kwenye kampuni mbili – Dowans na Richmond.
Mmoja wa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans katika nyaraka za sasa zilizopo ofisi ya usajili wa makampuni (BRELA), Brigedia Jenerali Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi amekana mara kadhaa kuifahamu kampuni hiyo.
Naye raia wa Canada, Andrew James Tice anayeonekana katika nyaraka za sasa za BRELA, aliwahi kuwa meneja uzalishaji katika kampuni ya Songas na baadaye kushika nafasi hiyo katika kampuni ya Richmond.
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali ambazo gazeti linazo, Tanesco na Dowans wamekubaliana kuwa maamuzi yoyote ya suala hilo, ni lazima yafuate sheria za Tanzania.
Ibara ya 14 ya mkataba wao inasema pamoja na suala hilo kufikishwa ICC, pale ambapo kutatokea mgogoro, bado sheria za ndani ya Tanzania zitatumika wakati wa kufikia utatuzi.
Ibara ya 17 ya sheria ya usuluhishi inasema, mara baada ya maamuzi husika kutolewa, yatasajiliwa na mahakama kuu na baada ya hapo itachukuliwa kuwa ni amri halali ya mahakama ya nchi.
Nchini Costa Rica, ambako Dowans inadaiwa kusajiliwa, hakuna rekodi zozote inazoonyesha kuwapo kwa kampuni hiyo.
"Dowans si kampuni halali ndani ya Costa Rica," inasema barua kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali nchini Costa Rica.
Barua hiyo ilisainiwa na Marianela Jimenez, Jumamosi ya 3 Agosti 2008 na kutumwa ofisi ya katibu wa Bunge la Jamhuri, saa 11:09 jioni ya siku hiyo.
Mmoja wa wanasheria nchini ameliambia gazeti hili kuwa serikali haistahili kulipa hata shilingi kwa Dowans kwa kuwa kampuni hiyo ilinunua mkataba kutoka kwa kampuni feki – Richmond.
Amesema, "Hata hatua ya Dowans Holding kuingiza kampuni ya Dowans Tanzania Limited katika madai yao, wakati wakijua fika kwamba kampuni hiyo siyo iliyosaini hati ya kuhamisha mkataba, ni kinyume cha taratibu na sheria za makampuni."
Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba kutoka kampuni nyingine yenye utata ya Richmond ambayo ilipewa kazi ya kufua umeme kuanzia Januari 2007 hadi Juni 2008.
chanzo Mwanahalis

0 Comments