[wanabidii] MwembeYanga yamkataa Lowassa kujiunga na CHADEMA na UKAWA

Monday, July 27, 2015
Zero torelance ya rushwa kwa CHADEMA ambayo ni mshirika mkuu wa UKAWA inamkataa Lowassa kujiunga na CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wake. Akihutubia katika mkutano wa siasa pale mwembe yanga, mwaka 2007, Dr. Slaa huku akisaidiana na Tundu Lissu, waliwataja mafisadi 11 katika nchi yetu. Orodha ya Dr. Slaa ya mafisadi ilijumuisha jina la Lowassa. Katika mkutano wa MwenbeYanga, CHADEMA ilitangaza zero tolerance kwa rushwa na ufisadi.

Tangu wakati huo, vita ya kupambana na ufisadi imekuwa sera kuu ya CHADEMA. Hata katika chaguzi za ndani za CHADEMA, rushwa haikubaliki kabisa na ni kigezo cha disqualification kwa wagombea. Sera hiyo kwa kiwango kikubwa imeifamya CHADEMA ipendwe na wanchinwengi na hivyo kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Hakuna hata siku moja ambapo CHADEMA imetangaza kuachana na sera yake ya kupambana na rushwa na ufisadi. Jaribio lolote na kumwingiza Lowassa CHADEMA kama mgombea ubunge au urais lina maana moja tu kwamba CHADEMA inasitisha rasmi vita dhidi ya ufisadi. Hivyo faida ya kisiasa ambayo CHADEMA na UKAWA ilikuwa nayo kupitia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi itakuwa imefikia tamati. Hakuna mantiki yoyote ya CHADEMA na UKAWA kupigana dhidi ya rushwa na ufisadi kama vile wizi wa ESCROW, mikataba ya kifisadi ya Gas na madini na nk.

huku wakimkumbatia Lowassa katika chama cha CHADEMA na UKAWA. Kwa ufupi, mantiki ya vita dhidi ya ufisadi inakufa na hivyo CHADEMA na UKAWA hawatakuwa na tofauti yoyote ya kisera na hivyo CHADEMA NA UKAWA watafanana na CCM.

Huu ni ukweli mchungu ambayo CHADEMA na UKAWA inabidi wauone. Kuna hatari ya CHADEMA na UKAWA kukosa kuungwa mkono na wanchi kama watafanya kosa la kumfanya Lowassa kuwa mgombea ubunge au urais kupitia CHADEMA au UKAWA. Kiukweli wataua visibility ya vipaji vya wanasiasa waliochipukia kama vile Mnyika, Tundu Lissu, Halima Mdee, Wenje, Msigwa, Vincent Nyerere, n.k. Hakuna hata siku moja ambapo CHADEMA wamewahi kumwondoa Lowassa kwenye List of shame.

Hawajawahi kumsafisha, na dhana hii ya kusafishana kwa dodoki, imepingwa sana na CHADEMA na UKAWA yake. Kuna vyama viko kama mafisi, vinasubiri CHADEMA na UKAWA wafanye kosa la kumkumbatia Lowassa. Vyama hivyo ambavyo ni kama mafisi wanaosubiri mkono wa binadamu udondoke ili waule vinajumuisha chama kile cha wasaliti waliotoka CHADEMA, yaani assosiation of cowards and traitors (ACT).

Share this :

Related Posts

0 Comments