[wanabidii] Hata kama huipendi CCM, lakini mikakati yake utaikubali! Hatimaye gamba lililokwama limejivua kiulaini kabisa

Sunday, July 12, 2015

Mwanasiasa wa Kiingereza aitwaye Winston Churchill aliwahi kusema, ''Courage is what it takes to stand up and speak; courage is also what it takes to sit down, listen and learn''.


Wazee wa CCM walifahamu ajenda kuu ya Uchaguzi mwaka huu itakuwa ni ufisadi na uwajibikaji.

Wazee wa CCM wakafahamu pia matarajio makuu ya wanaCCM ni kupata Mwenyekiti/Rais ambaye ni muwajibikaji.

Hata Mwaka 2012, baadhi ya wanaCCM walitaka kutenganisha kofia ya Mwenyekiti wa CCM-Taifa na Rais wa Tanzania kwa sababu walidhani Rais Kikwete hawajibiki ipasavyo katika kiti chake.

WanaCCM wengi wanaamini kukosekana kwa uwajibikaji ndani ya chama na serikali ndiyo kunasababisha hata ufisadi nchini na kuporomoka kwa chama.

Wazee wa CCM wakaiona hatari ya chama kuchukuliwa na Edward Lowassa ambaye alikuwa anatumia ajenda ya uwajibikaji katika kufikia malengo yake wakati alikuwa amezungukwa na watu wenye madoa ya rushwa na ufisadi.

Wazee wa CCM wakaamua kutafuta mbadala wa Lowassa ndani ya CCM katika hoja ya uwajibikaji ili hata kama watalikata jina la Lowassa, pawepo na mbadala kwa wanaCCM wanaovutiwa na historia ya utendaji wa Lowassa.

Wazee wa CCM wakamtafuta John Magufuli na kumuomba awe mgombea wa Urais wa Tanzania.

Siku ilipofika, Magufuli akaenda kuchukua fomu na kutembea mikoani kutafuta wadhamini huku akiwa ndani ya taratibu na Kanuni za chama. Kila alipoenda, aliongea kidogo huku matendo yakiwa ndani ya Taratibu na Kanuni za chama.

Kuna maeneo mengine alikuwa akifika anakuta baadhi ya viongozi wa CCM wameamua kufunga ofisi na kuondoka pamoja na kwamba amewataarifu kama atafika kusaka wadhamini. Wagombea waliokuwa wanatoa ahadi za vyeo na pesa ndiyo walikuwa wanakaribishwa kwa mikono miwili katika ofisi nyingi za CCM.

Wazee wa CCM wakawatafuta pia proxy solders kama kina Makongoro Nyerere ili kuhakikisha wanafuta sumu aliyokuwa anaiweka Lowassa katika sehemu aliyokuwa anapita kutafuta wadhamini. Wamepambana vitani wakisema wanataka chama chao kirudi kwenye misingi ya uanzishwaji wake.

Mkutano Mkuu lilikuwa ni hitimisho la kuvua magamba yaliyokuwa yanadaiwa yameng'ang'ania kiunoni ndani ya CCM.

Magamba yaliyokuwa kiunoni yamevuliwa na wazee wa CCM bila kumnyoshea mkono yoyote yule kiasi kwamba hata wale waliokuwa foot solders na agent wa magamba wamejikuta hawaamini kilichowatokea.

Proxy solders kama kina Makongoro Nyerere, kwa sasa wako kimya wanapata mvinyo kwenye vijiwe vya wazee wa CCM baada ya kukamilisha kazi waliyotumwa na Wazee wa CCM.

Mbatia hakukosea aliposema CHADEMA wasijifanye wanaweza kupambana na CCM peke yao, kufanya hivyo ni kuota ndoto za mchana kwa sababu watapata kichapo kikubwa kwa sababu CCM ni taasisi kubwa sana. Mbatia alimaanisha ukubwa wa CCM ni uwezo katika mikakati ya kisiasa.

Wapinzani wajipange upya kwa sababu katika macho ya wananchi, dhana ya ufisadi na uwajibikaji imejibiwa kivitendo na Wazee wa CCM katika Mkutano Mkuu wa CCM.

Hata kama huipendi CCM lakini ina darasa la kutufundisha kuhusu Mikakati ya Kisiasa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments