[wanabidii] BANZA STONE LEO KAFARIKI KWELI

Friday, July 17, 2015
BANZA STONE LEO KAFARIKI KWELI

Na Happiness Katabazi

MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Dansi nchini, Ramadhani Masanja "Jenerali Banza Stone " amefariki Dunia hivi punde nyumbani kwao Mtaa wa Sinza D,Dar Es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu na hivi sasa mwili wake unapelekwa kufadhiwa Hospitali.

Sisi watoto tuliokuwa na Banza Kata ya Sinza Dar Es Salaam, tuliishi vyema na Banza Kabla ajaanza kuugua na hadi alivyoumbukwa NA Maradhi.
Binafsi siku zote uwa name heshimu kubwa Banza pamoja na mapungufu yake ya kibo adabu ambayo yalisababisha Katika Uhai wake ajiingize Kutenda baadhi ya matendo Katika Jamii ambayo hayakutupendeza sisi wana Sinza wenzake na mashabiki wake wa muziki.

Daima Nitamkumbuka Banza,kwasababu Banza ni miongoni mwa watu mahususi walioshiriki kuitaka Kata ya Sinza kupitia taaluma yake ya muziki Kwani baadhi ya Nyimbo zake alikuwa eneo la Sinza Hali iliyosababisha eneo la Sinza Kuwa ni eneo maarufu sana.

Banza alikuwa ni rafiki mkubwa wa Kaka yangu Liston Mwesiga Katabazi.
Banza ulishindwa kwenda sambamba na Maudhuhi ya Wimbo wako wa KUMEKUCHA.Ndani ya Wimbo huo kuna maneno yake mayo ' Unapotaka kuanza Maisha Anza sasa usisubiri Kesho Kwani Utamkuta Mwana siwako Oooh,upatapo fahamu Jua Umepotea kweli Umepotea.

Wimbo huo naupenda sana kuliko Nyimbo zake zote alizowahi kuimba Banza.

Pole familia ya Banza na wapenzi wa muziki wa dansi na wakazi wenzangu wote tunaoshi Kata ya Sinza .

Mungu aiweke roho yake mahali panapostahili.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
17/7/2015.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments